Header Ads Widget

DKT. DUGANGE ATOA MWEZI MMOJA KITUO CHA AFYA MWANYA - KITEKO KUKAMILISHWA NA KUANZA KUTOA HUDUMA




OR TAMISEMI - KITETO


Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) ametoa mwezi mmoja kwa Mkurungenzi wa Halmashauri ya Kiteto kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mwanya kilichopo Kata ya Njaro wilayani Kiteto.


Ameeleza hayo jana tarehe 21 Februari 2023 wakati akikagua ujenzi wa kituo cha afya Mwanja uliopo katika hatua za ukamilishaji.


“Katika mwaka wa fedha mmoja wa fedha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia alileta Bilioni moja na milioni tisini kujenga vituo viwili vya Afya ambayo ni Mwanya na Kijungu pamoja na nyumba ya mtumishi 3in1 katika Halmashauri ya kiteto ambavyo vipo hatua ya ukamilishaji” amesema Dkt. Dugange


Dkt. Dugange amemuelekeza Mganga Mkuu wa Halmashauri kuhakikisha anatafuta vifaa tiba vya kuanzia ili huduma za awali kwa Wagonjwa wa nje (OPD) zianze kutolewa ifikapo tarehe 15/03/2023 kwa sababu ujenzi wa jengo hilo umekamilika.



Amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa milioni 590 kwa kata ya Njoro kwa ajili ya ujenzi Jengo la OPD, Maabara, Kichomea Taka, Nyumba ya Watumishi ya 3 in 1, Jengo la Upasuaji, Jengo la huduma yq Mama na Mtoto na Jengo la kufulia.


Aidha, Dkt. Dugange amesema Shilingi Milioni 900 tayari zimeletwa kwa ajili ya ukarabati wa hospitali ya Wilaya ambapo unafanyika ujenzi wa jengo la huduma za mama na mtoto, jengo la upasuaji pamoja na jengo la maabara katika hospitali ya Wilaya.



Kadhalika, Ameeleza kuwa gari la Wagonjwa na gari la usimamizi wa huduma za afya yatatolewa katika halmashauri ya kiteto ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI