Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuendelea kujitolea michango na Nguvu kazi kusaidia utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
Ameyasema hayo wakati wa ziara yake kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mtii miongoni mwa vituo vitatu ambavyo ujenzi wake unaendelea katika wilaya hiyo zilizopowe fedha na serikali jumla ya shilingi Bilion 1.5.
“Kwa dhati ya Moyo wangu niungane na wakazi wa Wilaya ya Same kuishukuru serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake kuhakikisha huduma ya Afya inaimarika na kutoa kiasi kikubwa cha fedha Kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma”. Kasilda Mgeni-DC Same.
Kwa sasa katika Wilaya ya Same kunaendea Ujenzi wa Vituo vitatu vua Afya kwenye kata za Miamba, Ruvu na Mtii ambapo kituo cha Afya Miamba pamoja na michango na nguvukazi toka kwa wananchi kituo hicho kimepatiwa kiasi cha Shilingi Milioni 500 fedha toka serikali kuu, pia vituo viwili vya Ruvu na Mtii vimepatiwa takribani Shilingi Milioni 500 kwa kila kimoja, fedha za serikali zilizotokana na Tozo.
Nao wananchi walio katika kijiji cha Mtii kunakojengwa Kituo hicho cha Afya wameipongeza serikali kwa kuwaunga mkono, kwakua kabla ya uamuzi huo wananchi hao walikwisha anza ujenzi wa Zahanati katika kijiji hicho, kwani wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya Kilometa 40 kufuata huduma za afya maeneo jirani na kuahidi kuendelea kukitolea michango na Nguvukazi.
"Ikitokea Dharura Mtu kuugua ghafla hasa mamazetu wajawazito tunapata usumbufu Sana, hapa hatukua na kituo chochote jirani unapoweza kukimbilia ndio maana tukaamua kuanza kujitolea ukenzi wa Hilo jengo hapo la Zahanati lakini chakushukuru zaidi no Serikali yetu kuona uhitaji tulionao na kutuletea mradi huu mkubwa kuona tunastahili kuwa na Kituo cha Afya na sio Zahanati".Alisema mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mtii kunakojengwa Kituo hicho cha Afya.
Nae mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anastasia Tutuba amesema kama ilivyo katika Mpango wa Serikali Halmashauri itaendelea kutenga sehemu ya fedha za makusanyo ya Ndani kumalizia Miradi vipaumbele hasa iliyoibuliwa na wananchi Kwa kujitolea michango na nguvukazi ili kuboresha huduma na pia Miradi mwingine ya Maendeleo.
0 Comments