Na Amon Mtega _Mbinga
BIDHAA zinazozalishwa na wazawa kwenye maeneo husika inatakiwa ziungwe mkono kwa kuzitumia bidhaa hizo ili kuongeza uchumi kwa wazawa hao pamoja na maeneo hayo kwa ujumla.
Hayo ameyasema na Joseph Mwambije ambaye ni balozi wa maji ya kunywa ya Asili (Asili Spring Water)yanayozalishwa na kampuni ya Mdaka Five Limited yenye makao yake makuu Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
Mwambije ambaye pia ni mwaandishi wa Habari Mkoani Ruvuma amesema kuwa kumekuwepo na baadhi ya wazawa wa maeneo husika kushindwa kuzikubali bidhaa zinazozalishwa kwenye maeneo yao hata kama zinaviwango vinavyotakiwa jambo ambalo hurudisha nyuma kimaendeleo kwenye nyanja ya uchumi kwenye maeneo hayo.
Balozi wa maji hayo amefafanua kuwa maeneo mengi yaliyoweza kuendelea kiuchumi hasa kwa wazawa wamaeneo husika ni kutokana na wazawa wa maeneo hayo kuwa wazalendo wa bidhaa za maeneo yao.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mdaka Five Limited Joseph Mdaka amesema kuwa maji hayo yanapatika Wilayani Mbinga katika chemuchemu za safu ya milima ya Mhekela.
0 Comments