MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson John ameitaka kamati ya magonjwa ya milipuko kutoa elimu juu ya magonjwa kulingana na mila desturi na tamaduni za eneo husika.
Ameyasema hayo Mjini Kibaha alipokuwa akifungua mkutano wa kamati hiyo inayoundwa na wanajamii, wataalamu wa afya, viongozi wa dini na kamati ya usalama ya Wilaya.
John amesema kuwa kwa kuzingatia hilo itasaidia kukabili magonjwa ya mlipuko kwa kutoa elimu juu ya kukabiliana na magonjwa hayo.
Kwa upande wake Johnson Mndeme kutoka Wizara ya Afya Idara ya Kinga sehemu ya afya kwa Umma amesema kuwa malengo ya kuanzishwa kamati hizo ni kutoa elimu juu ya magonjwa ya mlipuko ili kuepukana na dhana potofu
Mndeme amesema kuwa endapo elimu itatolewa mapema magonjwa hayo hayataenea na kuipunguzia gharama serikali kutibu wananchi hivyo kukinga itapunguza gharama hizo.
Kwa upande wake maganga mkuu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Peter Nsanya amesema kuwa wanakamati wanapaswa kutoa elimu ya kupambana na magonjwa mbalimbali ndani ya jamii.
Nsanya amesema kuwa jamii ihamasishwe kujikinga na magonjwa mbalimbali kwa kupata chanjo na kuyakabili magonjwa ya mlipuko ambayo yanaleta athari kwa muda mfupi.
0 Comments