MATUKIO DAIMA APP NA: FRANCO NKYANDWALE RUKWA.
Wanafunzi 2, 640 waingizwa katika mfumo rasmi wa shule katika Kata Nne kati ya Kata 97 Mkoani Rukwa kupitia Mradi wa Shule Bora unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikishana na Shirika la Maendeleo ya Uingereza UK AID.
Akifungua Semina ya Wandishi wa Habari Wilayani Nkasi mwanzoni mwa wiki Katibu Tawala wa Mkoa huo Rashid Mchatta amesema idadi hiyo ya wanafunzi kutoka mfumo usio rasmi inaiondoa Mkoa wa Rukwa katika mwamko duni wa kielimu na kuleta tija katika jamii.
Aidha Afisa Elimu Mkoa wa Rukwa Samson Hango amewambia Wandishi wa Habari kuwa kuwa matarajio ya uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali ni 42,666 na wameandikishwa kwa asilimia 88.64 na kwa darasa la kwanza wameandikishwa kwa asilimia 94.6 iwapo matarajio ni wanafunzi 46,036.
Afisa Elimu Hango amesema ili kuwafikia wanafunzi wanaotarajia kuandikishwa mbinu mbalizi zinatumika kuwafuatilia wanafunzi wenye sifa ya kuanza masomo hata wale wenye mahitaji maalumu kwa kupitia viongozi wa mitaa, Kata na viongozi wa Dini kuwashirikisha katika kutoa hamasa.
Mradi wa Shule Bora ni miaka sita (2021-2027) ambao unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa shirikiana na UK AID kwa gharama ya shilingi 270 bilioni ambapo mkikoa tisa inanufaika na mradi huo ambayo ni Rukwa, Kigoma, Mara, Simiyu, Sungida, Tanga, Dodoma, Katavi na Pwani.
Mradi wa Shule Bora utangia kuinua ubora wa Elimu jumuishi na mazingira salama ya kujifunzia kwa wavulana na wasichana.
0 Comments