Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) inatarajia kuanza kutumia Mfumo wa kielekroniki katika kusajili wanachama wa vyama vya ushirika.
Mfumo huo unaenda kutadhibiti na kuongeza uwazi katika usimamizi wa vyama vya ushirika na kuondoa changamoto ya Usimamizi katika Vyama vya Ushirika Nchini.
Akizungunza katika mafunzo yaliyojumuisha washiriki kutoka katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Vyama vya Ushirika Tanzania Valency Karunde alisema kuwa lengo la kusajili Vyama na wanachama kwa njia ya kielektroniki ni kuongeza Usimamizi na utunzaji wa kumbukumbu katika vyama hivyo.
“Tumelazimika kutoa mafunzo haya ya mfumo wa wasimamizi wa vyama vya ushirika wa kidigitali ambao ni mwendelezo wa jitihada za serikali kutoka kwenye makaratasi na kuingia katika mfumo wa Tehama”
“Unajua uhifadhi kwenye makaratasi hata udhibiti unakuwa mgumu ambapo tunaamini kuwa mfumo huu unaenda kupunguza gharama za uendeshaji wengi wanalazimika kusafiri ili kupata taarifa na vyama vikuu vinakuja Dodoma kuleta taarifa ujio wa mfumo huu hawatalazikika kusafiri” alisema Karunde
kwa upande wake Mwakiilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Frank Kanyusi alisema kuwa mfumo huo utaleta mapinduzi na kuleta nafasi ya ushrikka kujiendesha kidigitali hivyo kupunguza changamoto zinazokabili sekta hiyo.
“vyama vya ushirika vinapaswa vitumike kuchochea maendeleo kwa wakulima nchini ili kuwezesha sekta ya kilimo kuwa na mchango mkubwa kiuchumi matumizi ya mfumo huu yawe chachu ya watendaji wa ushirika kubadilika”
Nae Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha TAMCU Mussa Manjaule alisema kuwa katika mafunzo haya tunatarajia kutoka katika mfumo wa makaratasi na kuingia katika mfumo wa kidigitali.
“Kila chama cha msingi katika Wilaya ya Tunduru kina komputa isipokuwa mizani ya kieletronic bado lakini ndio tutaboresha ili tuendane na udigitali uliopo kwa sasa” alisema Manjaule.









0 Comments