Header Ads Widget

UBUNIFU WA VYANZO VIPYA VYA MAPATO WAHITAJIKA NJOMBE

 


Katibu Tawala wilaya ya Njombe Emmanuel George

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAAP Njombe


WAKATI  Halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani Njombe ikitarajia kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 ya zaidi ya shilingi bilioni 30.4 Serikali wilayani Njombe imeuagiza uongozi unaosimamia ukusanyaji mapato kuhakikisha unaongeza ubunifu katika kubuni vyanzo vipya vya mapato na umakini katika udhibiti wa mapato.


Katika kikao cha kamati ya ushauri  wilaya ya Njombe DCC kikiongozwa na katibu tawala wilaya ya Njombe Emmanuel George kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe amesema wataalamu wanapaswa kubuni miradi ya kimkakati,Kutengeneza mazingira ya fursa za kiuwekezaji pamoja na kuongeza nguvu katika usimamizi wa mapato ili kufikia lengo la kukusanya kiasi hicho cha fedha.



Awali kaimu Afisa Mipango wa halmashauri ya wilaya ya Njombe wakati akiwasilisha taarifa ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 Lwimiko Mellah amesema halmashauri hiyo inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.9 katika mapato yake ya ndani.


Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho cha ushauri cha wilaya akiwemo Mzee Lukule Mponji ambaye ni mdau wa maendeleo na Enaya Nyagawa wamehoji ni kwa namna gani wataalamu watakwenda kuboresha ukusanyaji mapato,namna ya kuepukana na athari za kimazingira kutoka na shughuli za kiuchumi pamoja na changamoto ya moto unaoteketeza maelfu ya ekari za miti.


Wakitolea ufafanuzi wa hoji mbalimbali za wajumbe hao baadhi ya maofisa wa halmashauri ya wilaya ya Njombe akiwemo kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo George Makacha na Ahmad Maguo mkuu wa idara ya Maliasili na Misitu wamesema changamoto ya moto inapaswa kuendelea kutolewa elimu kwa wananchi huku sheria zikizingatiwa katika utekelezaji wa shughuli zote.


Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Melkizedeck Kabelege amesisitiza ukaguzi wa magari ya mapato yanayopita katika mageti.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI