Tukio hilo lilitokea Leo majira ya Saa 2 asubuhi eneo la Semtema A Manispaa ya Iringa .
Rafiki wa karibu na marehemu Prince Salila mkazi wa Semtema A alisema kuwa mara ya mwisho alikuwa na msichana huyo na alimsimulia matatizo ambayo alikuwa anayapitia baada ya kupata mimba na kushindwa kuendelea na masomo yake.
“Mimi Winifrida ni rafiki yangu na jana nilikuwa naye pale dukani kwangu mpaka saa mbili usiku, na tuliongea mambo mengi sana na kushaurinana sana ila sikufikiria kama angefikia uamuzi huu wa kujinyonga kwani jana nilimshauri sana na saubuhi nilimpigia simu kumjulia hali kutokana na yale aliyonielezea kwani toka amepata mimba familia yake amemtenga na kumuana hana thamani tena” alisema Prince.
Petro Paulo Mdindile baba mzazi wa marehemu, amesema aligundua tukio la mwanae kufariki baada ya kuamka asubuhi na kumkuta akiwa tayari amesha jinyonga kwenye mti ambao upo nyuma ya nyumba yao, na kuacha mtoto wa mwaka moja akiwa anacheza na mdogo wake.
Hata hivyo akisimulia kabla ya kutokea kwa tukio hilo baba huyo alisema siku moja kabla ya kujinyonga (jana) binti yake alichelewa kurudi nyumban na akajaribu kumuonya kuachana na tabia hiyo ili aweze kusimamia malezi ya mwanae lakini hakufamahu kama binti yake alijisikia vibaya kutokana na maonyo hayo.
“Jana alichelewa sana kurudi nyumba, alirudi usiku na likuwa amemuacha mwanaye nyumba hapa na mimi ni kamuuliza alikuwa wapi na kumtaka kuachana na tabia hiyo ili kuweza kumlea mwanaye kwani ameshaanza kutembea hivyo anahitaji uangalizi sana” alisema Petro Mdindile baba wa marehemu.
Alisema Winfrida ameacha mtoto wa Mwaka mmoja na miezi 6 .
Mwenyekiti wa Semtema A, Rabi Samweli Mgata alimweleza mwandishi wa Matukio DaimaTv juu ya kutukio hilo na kutoa rai kwa wazazi na walezi kuwa karibu na Watoto wao kwanzia shuleni hadi nyumbani kwa kufuatilia maendeleo yao pamoja na kujua changamoto zinazo wakabili ili kuweza kuwaepusha na matukio hatari ambayo yamekuwa kiwakuta Watoto wengi kwa sasa.
“Wazazi wengi wamekuwa bize sana mpaka wanasahau wajibu wao kwa Watoto jambo ambalo linapelea Watoto wengi kuharibika hivi sasa maana ikifika jioni utakutana na mabinti wadogo wanazurura huku mtaani na nguo za ajabu alafu wazazi hawana Habari kabisa hivyo kama utaona mtoto amekushinda ni bora ukatafuta wataalam wakaongea naye ili kuweza kuwanasuru na majanga ila siyo kuwa mkali kupita kiasi au kumtenga” alisema mwenyekiti huyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi alipotafutwa Kwa Njia ya simu hakupatikana zaidi ya simu yake kuita bila kupokelewa .
0 Comments