Header Ads Widget

MNEC MLAO AHITIMISHA ZIARA YAKE KANDA YA ZIWA KIBABE

 




Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Cde. Ramadhan Mwinshehe Mlao (MNEC) amewasili mkoani Geita akitokea mkoani Mwanza ambapo amepokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Geita Cde. Manjale Lyabugu Magambo katika wilaya ya Mbogwe.


MNEC Mlao ametembelea na kufungua mashina ya wakereketwa wa CCM pamoja na kupandisha bendera ambapo amefungua shina namba  moja la bodaboda Kata  ya Nyakasuru, pia shina namba mbili la wakereketwa ambao Ni madereva wa magari madogo na bajaji  katika Stendi ya Idalafuma na Shina namba tatu la wakereketwa wajasiriamali katika soko la Kilimahewa.


Aidha MNEC Mlao amewajulia hali wagonjwa katika kituo Cha Afya Masumbwe na kuwashika mkono na akiwa hospitali ya Mbogwe MNEC Mlao ameshiriki na wauguzi wa hospitali tukio la kukakata keki na kumtakia heri pamoja na fanaka ya kuzaliwa Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Zaidi MNEC amesema katika kusherekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mh. Rais Dkt. Samia tuzidi kuendelea kumuombea kwa Mungu ili apate Afya tele na kuendelea kulilietea taifa letu la Tanzania maendeleo zaidi.



Pia MNEC Mlao amefanya Mkutano wa ndani katika ukumbi wa Casablanca uliopo kata ya Nyakafuru ambapo katika mkutano huo MNEC Mlao amewashukuru wanachama wa CCM mkoa wa Geita kwa mapokezi mazuri na ya heshima na amewataka Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mstari wa mbele kuyasema mambo mazuri ambayo mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na ameendelea kuyafanya ikiwa pamoja na kutoa fedha za miradi ya kimaendeleo Shilingi bilioni 375.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI