Header Ads Widget

MIKUTANO YA HADHARA NI FURSA YA KUONGEZA UCHUMI.

 


NA CHAUSIKU SAID__MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Katibu wa chama Cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria Zacharia Thomas ameeleza kuwa kufanyika Kwa mikutano ya hadhara ni fursa ya kuongeza uchumi katika Nchi.


Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mkutano utakaofanyika tarehe 23 katika viwanja vya furahisha Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.


Thomas ameeleza kuwa mzumguko mkubwa wa fedha utapatikana kutokana na mikutano ya adhara inayoanaza kufanyika na wananchi kuendelea kuingiza kipato kama ilivyokuwa awali.


"Kila mwanachi Kwa sasa ataanza kuingiza faida moja Kwa moja kutokana na wageni wote wanaoingia kutoka Mikoa tofauti tofauti na mzunguko wa fedha utaendelea kuonekana" Alisema Thomas.


Ameeleza kuwa chama hicho kitajikita katika kusajili wanachama wake katika Mfumo wa kidigital na kuhakikisha wanawapa kadi zao hapa hapo ambapo Mfumo huo itawasaidia kufahamu idadi ya wananchama walio nao


Aidha amewahakikishia wananchi wote kuwa  wamaejipanga kufanya mikutano yote ya kisiasa isiyo na vurugu na kufanyika Kwa amani na utulivu itakayofata sheria ya Nchi.


Hata hivyo Kwa hatua nyingine wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Kwa kutii sheria ya kufanya mikutano ya adhara kitu ambacho hakikufanyika Kwa muda wa miaka Saba.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI