Header Ads Widget

KILIO CHA BARABARA YA LIBIKILIFIMBILE KWA WAKAZI WA JIMBO LA MADABA -WINO KUKAMILIKA.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Theofanes Mlelwa Akizungumzia kuhusu maendeleo yanayofanywa kwenye Halmashauri hiyo.
Kaimu meneja wa Tarura Songea mhandisi Godfrey Mngale akielekeza namna ujenzi wa barabara ya Libikilifimbile unavyoendelea.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Amon Mtega, Madaba.

KILIO Cha muda mrefu cha Wakazi wa kata ya Wino Jimbo la Madaba Mkoani Ruvuma cha kuhitaji kupatiwa barabara ya kutoka kwenye kata hiyo hadi makao makuu ya Halmashauri ya Madaba kimesikika ambapo tayari barabara hiyo imeanza kufanyiwa kazi.


Akizungumzia barabara hiyo  mbele ya Mbunge wa Jimbo la Madaba Dkt Joseph Mhagama diwani wa kata ya Wino ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Theofanes Mlelwa amesema kuwa barabara hiyo itakuwa ukombozi kwa Wananchi hao  na kuwa kilikuwa ni kilio cha muda mrefu.


Mlelwa amesema kuwa barabara hiyo ambayo inatambulika kwa jina Libikilifimbile ikikamilika itaunganisha na barabara inayoenda Madaba ambako ndiko makao makuu ya Halmashauri jambo ambalo amesema litawapunguzia adhaa Wananchi kutembea umbali mrefu.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Joseph Mhagama akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo amesema kuwa anawapongeza  Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Wilaya ya Songea kwa kutenga bajeti kwaajili ya ujenzi wa barabara hiyo.


 Mbunge Dkt Mhagama amesema kuwa barabara hiyo ameipigania kwa muda mrefu na sasa imeshaanza kutekelezwa na kuwa licha ya kuwapunguzia adhaa Wananchi lakini bado itaimarisha uchumi kwa Wakazi wa Jimbo hilo pamoja na Serikali.


Amefafanua kuwa katika Jimbo hilo tayari barabara mbalimbali zinazounganisha toka eneo moja hadi lingine nyingi zimefanyiwa kazi na kuwa zote zitaunganishwa ili kufanikisha kuendelea kuimalisha chumi.


Naye kaimu meneja wa Tarura Songea mhandisi Godfrey Mngale awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwenye Jimbo hilo amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 miradi mitano itatekelezwa na fedha zitakazotumika ni zaidi sh. Bilion 1.9 ikiwemo na barabara ya Libikilifimbile.


Akizungumzia kuhusu barabara ya Libikilifimbile mhadisi Mgale amesema kazi inaendelea na kuwa kwa sasa linajengwa boksi kalavati ambalo litagharimu zaidi sh.Milion 72 .5 ambalo linajengwa na kampuni ya Luke Associates Limited ambayo ni yamzawa wa Ruvuma.


Mhandisi huyo amesema kazi inaendelea na kuwa mkandarasi ypo saiti anaendelea na kazi hivyo amewaka Wananchi kuwa na subira kuwa tatizo la barabara hiyo kinaenda kuisha huku akimpongeza Mbunge Dkt Joseph Mhagama kwa kuifuatilia barabara hiyo kwenye ofisi za Tarura mara kwa mara.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI