Header Ads Widget

ZAIDI YA ASILIMIA 70 YA UMEME UNAOZALISHWA HAPA NCHINI HUTUMIA GESI ASILIA.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Rashid Chuachua
Afisa TPDC Eva Swillah

                                                           xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

 Na Amon Mtega,Mbeya.

IMEELEZWA kuwa zaidi ya asilimia 70 ya umeme unaozalishwa katika gridi ya Taifa unatokana na gesi asilia ambayo inapatikana hapa Nchini Tanzania kwa usimamizi wa Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).


Hayo yamesemwa na mkuu wa Wilaya ya Mbeya  Rashid Chuachua wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa semina ya waandishi wa habari kuhusu tasnia ya mafuta na gesi asilia.


Mkuu huyo  akizungumza kwenye ufunguzi wa semina hiyo ambayo washiriki ni waandishi wa habari kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini amesema kuwa gesi asilia imekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo kwa Taifa hapa Nchini hasa kwenye sekta ya umeme.


Dkt Chuachua amefafanua kuwa licha ya gesi hiyo kutumika asilimia zaidi ya 70 kwenye umeme lakini bado imekuwa ikitumika kwenye Nyumba, magari pamoja na kwenye viwanda mbalimbali.


 Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga vema katika kuitumia gesi asilia ambayo itatumika na kwenye miradi mikubwa 19 ya kimkakati ikiwa dira ya maendeleo ya Taifa 2025 na mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano (5)  ambayo kati ya hiyo miradi tisa(9) inatekelezwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Nishati ikiwemo miradi minne(4) inayotekelezwa na  kupitia TPDC .


 Ameeleza kuwa miradi inayotekelezwa na TPDC ni mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimininika (LNG) unaofanyika Kijiji cha Likong'o Mkoani Lindi, mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika mashariki (EACOP)ufuatiliaji wa mafuta katika bonde la Eyasi Wembere na mradi wa utafutaji wa gesi asilia katika kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini ambapo mpaka sasa miradi hiyo yote ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


Kwa upande wake mmoja wawezeshaji ambaye ni Afisa wa TPDC ,Eva Swillah amesema kuwa mpaka sasa kiasi cha gesi asilia kilichogundulika ni futi za ujazo tirioni 57.54 ambapo sehemu ya kiasi kilichogundulika kinatumika kwenye miradi mbalimbali.


Afisa Swillah amesema kuwa hadi sasa zaidi ya Nyumba 1500 na magari 1500 yameunganishwa na gesi asilia na inatumika vizuri huku ikiwa imesaidia kupunguza gharama kwa watumiaji na kuwa shirika limejipanga kuendelea kusambaza mabomba ya gesi asilia katika mikoa mingine kwa kasi zaidi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI