NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
Ofisi ya waziri mkuu kitengo Cha maafa imetoa mafunzo ya utayari na uokoaji kwa siku 7 kwa wavuvi 344 mkoani Kagera ili kuimarisha uzalendo na utayari miongoni mwao pindi yanapotokea madhira majini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri mkuu Menejimenti ya Maafa, Prudence Constantine akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo katika mwalo wa Kateme Magarini ulioko wilayani Muleba mkoani kagera ambapo amesema kuwa vikundi vya wavuvi vilivyopatiwa mafunzo vimetoka Bukoba Manispaa, Misenyi na Muleba ni katika visiwa vya Goziba,Bumbile, Mazinga na Mwalo wa Magarini.
"Tunawashukuru viongozi wetu wa kitaifa kwa kuona umuhimu wa kuendesha mafunzo haya maalumu ya utayari katika uokoaji kwa wavuvi wetu ambao walishiriki katika uokoaji wa watu 29 katika ajali ya Precion Air kwa kutumia njia zao za kiasili ndipo waziri mkuu akaagiza wavuvi hawa wapatiwe mafunzo ya kitaalamu ya uokoaji na sisi tumefanya hivyo kwa maelekezo yake kwa kuanzia mkoani kagera ambapo jumla ya wavivi 344 wamepatiwa mafunzo hayo na wako imara kukabiliana na majanga endapo yatatokea"
"Baada ya mafunzo haya vijana wameonekana kuwa na muamuko mkubwa na wamefurahia mafunzo hayo kwani walikuwa hawaamini kama wanaweza kupatiwa mafunzo haya, hivyo wameiona kama fursa kwao na sasa wameiva"
Ameongeza kuwa mafunzo ya uokozi yameanzia mkoa wa Kagera lakini kuna mpango wakuendelea kutoa mafunzo maeneo yote yenye nyuso za maji ikiwa ni pamoja na mkoa wa Mwanza, Geita, Mara na Kigoma.
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Kagera, Toba Nguvila ameendelea kuwashukuru wavuvi wa mkoa Kagera kwa jitihada walizozifanya za kuokoa abilia 26 waliokuwemo kwenye ndege ya Precion Air iliyopata ajali mnamo Novemba 6 mwaka huu huku akiwatahisi kutumia mafunzo pamoja na vifaa walivyokabidhiwa kujikinga wenyewe na kuwaokoa wengine na kuacha mazoea ya kwenda ziwani bila kuvaa 'life jackets'.
"Inawezekana wengine mnajua kuongelea na wengine wanatumia vyombo lakini wengi wenu mnapoingia kwenye maji kwaajiri ya uvuvi mnatembea bila vifaa vya kujikinga inapotokea dhoruba mmekuwa mkipata changamoto sana ndiyo maana serikali iliona kuna umuhimu wa kutoa mafunzo ya kuwajengea ujuzi katika uokozi yakiendana na utoaji wa vifaa hivi kwenu wavuvi kwaajiri wa kujiokoa wenyewe na kuwaokoa wengine ajali inapotokea, vifaa hivi mvitumie viwasaidie katika kukabiliana na majanga haya"
Naye mkuu wa wilaya ya Muleba, Kemilembe Rwota amewasihi wavuvi waliopata mafunzo hayo kuwa mabalozi kwa wavuvi wengine ambao hawakupata nafasi ya kushiriki katika mfunzo hayo huku akiwataka kutumia vifaa vya uokoaji walivyokabidhiwa kwa matumizi lengwa na sio kuviuza.
"Itakuwa sio jambo zuri mpewe vifaa vya uokoaji leo alafu kesho tusikie kuwa kuna mtu ameuza vifaa hivi na kwa yeyote atakayebainika kuuza vifaa hivi hatua za kisheria zitachukuliwa juu yake"
Mafunzo hayo yalifunguliwa mnamo Novemba 28 mwaka huu katika Manispaa ya Bukoba yakijumuhisha wavuvi kutoka Manispaa ya Bukoba na Misenyi na yamehitimishwa katika Mwalo wa Magarini ulioko wilayani Muleba Mnamo Desemba 4 mwaka huu.










0 Comments