Header Ads Widget

OFISI YA WAZIRI MKUU YARIZISHWA KUENZIWA MWALIMU NYERERE KWA VITENDO

 



Na Shomari Binda-Musoma


OFISI ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) imeonyesha kuridhishwa na namna Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,anavyoenziwa kwa vitendo katika upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Kasper Mmuya, wakati wa upandaji wa miti ya matunda kwenye shule ya msingi Mwisenge aliyosoma Mwalimu Nyerere ikiwa ni kuelekea mkutano wa lishe. 


Amesema ametembelea mashamba ya mfano kwenye shule hiyo na kuona namna jitihada mbalimbali zinazofanywa na walimu pamoja na wanafunzi katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.


Naibu Katibu Mkuu huyo amesema yanapojadiliwa masuala ya lishe suala la matunda ni sehemu na imepelekea ofisi ya Waziri Mkuu kutoa miti 300 kwenye shule hiyo ili iweze kupandwa na kuboresha lishe. 



" Tumefurahi kufika kwenye shule hii ya Mwisenge ambayo inakumbukumbu nzuri ya taifa letu na tumelizidhishwa namna  ambavyo Mwalimu anaenziwa. 


" Tupo hapa kwaajili ya mkutano wa lishe na tumekuja na miti ya matunda na mbegu za mbogamboga tukiamini ikipandwa na kutunzwa itakuja kuboresha lishe na kuwa na afya bora",amesema Mmuya.


Akipokea miti hiyo pamoja na mbegu za mbogamboga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara, Meja Jenerali, Suleimani Mzee, mkuu wa wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfan Haule, amesema miti na mbegu zilizotolewa itasimamia vizuri na kuhakikisha inakua na kufikia lengo husika. 


Amesema miti hiyo ya matunda itasambazwa kwenye shule na taasisi mbalimbali ili iweze kupandwa ili iweze kuwa sehemu ya lishe. 



Aidha akifungua mkutano wa 8 wa mwaka wa wadau wa lishe mjini Musoma, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu( Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya,amesema hali ya lishe nchini inaendelea kuimalika kutokana na kupungua kwa udumavu.


Amesema mikakati ya kupambana na afua za lishe inaendelea ambapo licha ya udumavu kupungua wapo watoto milioni 3 ambao wana udumavu na mikoa 11 ina tatizo hilo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI