Header Ads Widget

WAOMBA KUFANYIWA UPASUAJI WASIHARIBU MAUMBILE YAO.

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma 


UPASUAJI kwa Mwanamke anayejifungua mara nyingi hufanyika kwa sababu maalumu endapo ikatokea mama kujifungua kwa kawaida kunaweza kuhatarisha uhai wake au mtoto. 


Na hivyo ndivyo ilivyokuwa imezoeleka miaka yote tangu enzi za mabibi na mababu zetu. 


Lakini sasa hivi maisha ya utandawazi yanaonekana kuleta mabadiliko makubwa. 


Imeshuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni kuwepo kwa wimbi kubwa la baadhi ya kina Dada hasa wadada ambao wanaigia kwenye umama kuomba kufanyiwa Upasuaji wakati wa kujifungua wakihofia uchungu na wengine wakidai kuwa maumbile yao kuharibika na hivyo kutopendwa tena naweza wao


Manasseh Muhumpa ni Mkazi wa Kata ya Mkonze Dodoma amesema  Wanawake wengi wanapenda njia hiyo ya upasuaji kwa woga wa kukabiliana na adha ya uchungu na maumbile yao kuharibika wengi hudai kuwa hali hiyo inafanya mwanaume/Wanaume kutowapenda tena kama awali.


Pia amesema hofu ya kukandwa maji moto kama wazazi wetu wa zamani Wengi kudhani maumbile yao ya mwili yataharibika na kutovutia kama awali.


"Hiyo yote inasababishwa na Wadada wa kisasa kutokupatiwa mafunzo ya kimila Kama vile (UNYAGO) hali ingewafanya kujitambua nakujithamini," alisema Muhumpa


Amesema Wadada wengi wamekuwa hawajitambui thamani yao nakuona ni kitu cha kawaida na kimekaa kibiasha kumbe ni Utu huku wengine wakiishi kwa hadithi zisizo na kweli wala mashiko juu ya uzazi wa njia ya kawaida kuwa  wakizaa kwa njia hiyo atapata (saratani ya njia ya kizazi).


Hata hivyo amesema shida hiyo ipo sana kwa wadada waliokeketwa kwani hofu yao kubwa ni wakati wa kujifungua wamekuwa wakiwapa shida watia huduma hali inayopelekea kulazimisha kufanyiwa Oparetion.


"Niukweli usiopingika wanawake waliokeketwa wanapojifungua huwa wapo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kwani humwaga damu nyingi," amesema.


Hata hivyo kutokana na utandawazi kumeibuka wadada wengi  kujishirikisha na mapenzi ya kinyume na maumbile hivyo kuhofia masaibu ya aibu kipindi cha kujifungua hivyo kuomba kupasuliwa wakati wa kujifungua ili kuficha tabia yake mbele ya jamii na kwa wakunga na madaktari


Asha yuba Mgalula ni mkazi wa mailimbili Dodoma ni mama wa Watoto wawili anasema  asilimia kubwa ya Wadada wanaomba kuzaa kwa upasuaji ni wale wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile


Anasema Madaktari huwa wanasema mapenzi kinyume na maumbile kwa mwanamke na Wadada ni hatari kwani wakati wa kujifungua Mtoto badala ya kutoka sehemu husika anakwenda kutokansehemu ya haha kubwa hii ninhatari


"Kama tunavyoona na kushuhudia mambo ya ajabu yanayoendelea mapenzi ya kinyume na maumbile ndio hahaari ya Mjini kinadada Sasa wanaposhika ujauzito inakuwa ngumu yeye kuzaa kawaida hivyo njia lahisi kwake nikufanyiwa upasuaji ,"


Neema Hoza ni mama mwenye Mtoto wa Mika 2 ambaye pia alizaa Mtoto huyo kwa njia ya upasuaji ambapo aliomba kujifungua Mtoto wake huyo kwa njia ya upasuaji (Oparetion).


Anasema kwa Upande wake hakutaka kuzaa mwanae kwa njia ya maumivu na ndio Maana aliamua kuzaa kwa njia ya kufanyiwa Upasuaji


"Sikutaka kuzaa kwa njia ya kawaida kwani sikuhitaji kupata maummivu Kama wanavyo zungumzia Wanawake wengine waliowahi kujifungua kwa njia ya kawaida kwamba uchungu unauma, " alisema ," amesema Neema.


Anasema katika Karne yasasa ni jamani la kawaida mtu kuomba kufanyiwa upasuaji anapokaribia kujifungua  kwani ni ukweli kwamba njia ya upasuaji ndio njia salama.


Jamii usema kuwa mzazi aliezaa Mtoto bila uchungu eti mzazi huyo huwa hana mapenzi sana na Mtoto huyo kwasababu hajazaa kwa uchungu kama wanawake wengine Neema ameeleza kuwa kwake ipo tofauti kwani anampende mwanaye mpaka anahisi kuumwa.


"Hahahaaaaa kwanza nicheke kidogo mapenzi nilikuwa nayo kwa mwanagu hayaekezeki labda nikwambie kitu mtu hawezi kubeba mimba miezi tisa halafu uje uzae Mtoto umchukie basi  mtu wa hivyo atakuwa na matatizo ya akili," amesema Neema


Na kuongeza Kusema "Yani iko hivi huwezi kusema eti mimi niliomba kuzaa kwa upasuaji sina mapenzi na mwanagu sio kweli vile kubeba Mimba miezi tisa ni mapenzi tosha," amesema


Alipoulizwa labda jamii ilimchukuliaje  alipoomba kuzaa kwa uparesheni Neema anasema "Mimi ni mtu ambaye siangalii jamii inanitazamaje kwani ukweli ni kwamba upasuaji ndio njia salama kikubwa nikufuata masharti nanushauri wa Daktari kwa kuhakikisha unafanya mazoezi na kuacha kudekadeka eti tu unakidonda," amesema Neema.


Naye Atuka Hussein Ally anasema alizaa mtoto wake wa kwanza mwenye umri wa miaka 5 kwa njia ya upasuaji baada ya Madaktari wa Hospitali ya KCMC kushauri njia hiyo ingemsaidia kumpata Mtoto wake.


"Nilifikishwa Hospitali ya KCMC nikiwa katika hali mbaya kidogo nikitokea jiini Arusha baada ya kucheleweshwa kufika ndipo Madaktari walisema natakiwa kupasuliwa," amesema Atuka

 

Na kuongeza Kusema" Kiukweli sikuwaza Kama ningekuja kuzaa Mtoto wangu wa njia ya uparesheni yani upasuaji lakini kutokana na hali yangu nikiofikanayo hospitalini pale  nililazimika kufanyiwa ili mimi na mtoto tuwe salama na nimekiri kuwa njia hii ni salama," anabainisha 


Aidha alipoulizwa kwa mtazamo wake anadhani kujifungua kwa upasuaji ndio njia salama tofauti na kujifungua kwanjia ya kawaida atukaa anasema  kila mtu na mtazamo wake "Mimi leo ukiniambia nizae kwa njia ya kawaida si dhani kama nitaweza kwa maana nimeshazoea kuzaa kwa kisu .


Hata hivyo anabainisha kuwa hata sasa akibahatika kupata ujauzito mwingine atakwenda kuzaa kwa upasuaji kwani ndio njia anayoiona salama kwake.


Nasra Mkwambe ni mama wa mtoto mmoja ambaye yeye alimzaa mtoto huyo kwa njia ya kawaida anaeleza anawashanga wasichana wa sasa kujitafutia maradhi wasiokuwa nayo kwa kulazimisha kuwa na matatizo katika miiliyao.


Suala la kufanyiwa upasuaji huko nyuma kwa mabibizetu na mababu zetu hazikuwepi na hata kama zilikuwepo ilikuwa ni kwenye shida tu tofauti na ilivyo Sasa eti mtu unalazimisha kufanyiwa upasuaji.


Anasema ukifanyiwa upasuaji ni ubovu tosha maana kile kidonda huwa hakiponi haraka miaka nenda rudi mpqka kufa kwako nitoe tu ushauuri kwa akinadada ujana na utandawazi utatuumiza na tusipende mambo ya kuiga .


WATAALAMU WA AFYA WANVYOSEMA


Wataalamu wa masuala ya afya wanakiri kuwepo kwa sababu kadhaa ya kuibuka kwa tabia hiyo:


Kulinda maumbile


Dhana ya baadhi ya wanawake wanaokwenda kujifungua kuomba au kutaka kufanyiwa upasuaji kwa kuhofia kubadilika maumbile yao huku wengine wakihofia uchungu wa kujifungua.


Dkt. Abel  Ikwasa Ikwasa ambae ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika Hospitali Kuu ya Rufaa Dodoma amesema hali hiyo kwa sasa inaonekana ya kawaida. 


Dkt. Ikwasa amesema wapo kina mama wajawazito ambao wanaotaka kuzaa kawaida huku wengine wakitaka kujifungua kwa njia ya upasuaji kutokana na sababu zao binafsi. 


Anaendelea kusema kuwa baadhi ya nyakati wamekuwa wakipokea wagonjwa ambao wana matatizo ya kiafya hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji.


"Wanawake wengi wamekuwa wakija na mawazo ya kutaka kufanyiwa upasuaji, na sisi madaktari tumekuwa tukiwapa ushauri na tunafurahi kwamba baadhi wamekuwa wakikubali kuzaa kwa njia ya kawaida lakini wengine wanakataa.


"Ukweli ni kwamba kujifungua kwa njia ya upasuaji sio salama sana  hivyo niwaombe tu wasisikilize maneno ya marafiki kwamba kuzaa kwa upasuaji kunaharibu maumbile yao," amesema Dkt Ikwasa.


Changamoto tunayokumbana nayo ni  pale anapokuja mzazi mwenye shida na nil azima afanyiwe upasuaji na yeye hataki kufanyiwa upasuaji kisa tu ameambiwa ni marufuku kuzaa kwa upasuaji na wana familia. 


"Tunapopata mgonjwa wa hali hii kwa kweli huwa shida kidogo kwani mpaka uanze kumuelimisha inakuwa kazi kidogo," amesema Dkt Ikwasa. 


Hata hivyo ametoa ushauri kwa kina dada hasa wale wanaozaa kwa mara ya kwanza waache kudanganyana kwani  wamekuwa wakiambina kuwa ukizaa kawaida maumbile yanabaadilika , wengine kuhofia uchungu kuuma wengine kukandwa maji ya moto huo sio ukweli ni kwamba njia salama kabisa ya kujifungua nikuzaa kawaida.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS