Header Ads Widget

ASHANGAZA MAHAKAMA BAADA YA KUJARIBU KUONYESHA SEHEMU ZAKE ZA SIRI

Mfanyabiashara anayekabiliwa na madai ya ulaghai aliwashangaza waliohudhuria Mahakama hapo jana Jumatatu, Desemba 19 baada ya kujaribu kuonyesha sehemu zake za siri mahakamani hapo akidai kuwa alipigwa na maafisa wa polisi kutoka Kituo Kikuu cha Polisi jijini Nairobi baada ya kukamatwa.


Clement Odera almaarufu Hamisi alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Milimani, Micheni Wendy kwa tuhuma za kula njama ya kumtapeli mtu anayetafuta kazi.


Kulingana na shtaka, Odera kati ya Novemba 1, 2021 na Oktoba 25, 2022 alikula njama na mtu mwingine ambaye bado hajakamatwa ili kumlaghai Christopher Nyalenda Sino kiasi Cha pesa Ksh1,866,000 kwa kusingizia kwamba angemsaidia kupata kazi katika Idara ya Mahakama.


Inasemekana mshtakiwa alipata pesa hizo kwa kisingizio cha uwongo kwamba angemrahisishia kupata kazi ya udereva kwa vile alikuwa na uhusiano na kamishna katika Tume ya Huduma za Mahakama (JSC).


Mwanaume huyo aliishangaza mahakama kwa kujaribu kuishusha suruali yake akimweleza hakimu kuwa sehemu zake za siri zilikuwa zimevimba kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupigwa na askari polisi wakimlazimisha kukiri kosa.


"Heshima yako, nilichapwa sana na hao askari. ata nikikuonyesha sehemu zangu za siri zimevimba. Nilipigwa nikiambiwa nikubali makosa (Mheshimiwa nilipigwa na askari polisi, nikikuonyesha sehemu zangu za siri zimevimba, walinipiga na kuniambia nikubali kosa hilo," alisema mshitakiwa mahakamani hapo.


Kufuatia maelezo ya mshitakiwa huyo, Hakimu aliamuru azuiliwe katika Kituo Kikuu cha Polisi ili kurahisisha kupelekwa hospitalini hapo kwa uchunguzi wa afya yake. Mahakama pia iliamuru afisa mpelelezi kutoa ripoti ya matibabu kwa mahakama.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS