Wajasiriamali tumieni mitandao kujitangaza ili mpate wateja wengi fanyeni biashara zenu kisasa kwakutumia mitandao.
Kauli hiyo ameitoa mkuu wa wilaya ya mtwara dunstan kyobya wakati akikabidhi hundi ya zaidiya shilingi milioni 244 kwa vikundi 35 vya ujasiliamli vilivyoomba kupata mkopo wa makundi ya wanawake, walemavu na vijana ambapo alisema kuwa watu wengi wapo kwenye mitandao.
“Nimpongeze Mkurugenzi Manispaa ya Mtwara Mikindani Kanal Emmanuel Mwaigombeko kwa mafunzo ya siku tano aliyoyatoa kwa vikudi 35 vilivyokopa kabla ya kupewa mkopo huo”
Dunia ya leo kila kitu kipo kwenye mtandao ukiweza kupiga picha kila unachofanya na ukatangaza unaweza kufanikiwa zaidi na kupata wateja zaidi jifunzeni kuongeza mtandao wa biashara zenu” alisema Kyobya
Nae Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Shadida Ndile alisema kuwa mikopo hiyo ni mapato ya ndani hivyo wanapoko warudishe ili na wengine waweze kukopa.
“mkatumie pesa hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na serikali rudisheni fedha hizo kwa muda uliopangwa mnaweza kupata tena hakikisheni haziwagombanishi”
Nae Zuhura Juma diwani wa viti maalum manispaa ya mtwara mikindani alisema kuwa vikundi vyote viliomba na kupewa kwa wakati hata marejesho yawe kwa wakati.
Mikopo inatolewa kwa wakati na irejeshwe kwa wakati wengi wengu mnatabia ya kulalamika mnapochukuliwa hatua wanawake wengi wanaaminika wanakopa na kurejesha kwa wakati niwashauri tu Vijana muige mfano wa wanawake wanachukuwa kwa wakati wanarejesha kwa wakati”








0 Comments