Header Ads Widget

UVCCM MOSHI VIJIJINI WAWASHUKIA WANAOHOJI DENI LA TAIFA.



NA GIFT MONGI,MATUKIO DAIMA APP,MOSHI


Kwa siku za karibuni kumeibuka mijadala katika baadhi ya mitandao ya kijamii na makundi zogozi juu ya ukubwa wa deni la taifa na hatma yake Kwa taifa kwa siku zijazo.


Kutokana na mjadala kuwa mpana zaidi kukamsukuma waziri wenye dhamana ya fedha na mipango Dkt Mwigulu Nchemba kutolea ufafanuzi suala lenyewe ambapo alisema bado ni stahimilivu na kuwa bado halina madhara kama inavyotaka kuaminishwa.


Alisema kama taifa bado linakopesheka na kuwa hakuna mtu ambaye atakuja kufuatwa nyumbani ili akalipe au achangie kulipa deni la taifa na kuwa bado elimu inahitajika zaidi ili watu waweze kuelewa nini maana ya deni la taifa.


"Sisi tunakopesheka na ndio maana tukiona sehemu ina fursa tunafanya hivyo maana tayari tunakidhi vigezo ingekuwa ni kinyume cha hapo tusingeaminika na kupewa  mikopo hiyo"alisema Dkt Mwigulu


Wakati Waziri huyo akitoa ufafanuzi huo umoja wa vijana wa  Chama cha Mapinduzi. (UVCCM)  wilaya ya Moshi Vijijini umekuja juu na kudai kumekuwepo na propaganda katika mambo ambayo ni nyeti kwa ustawi wa taifa.


Mwenyekiti wa umoja huo Yuvenail Shirima amesema tatizo kubwa ni baadhi ya watu kutojua kile kinachozungumzwa na badala yake kudandia hoja kwa lengo la kupata huruma kwenye ulingo wa siasa.


"Wapo vijana naona wanahangaika na deni la taifa ila ninachokifahamu ni kutafuta huruma za kisiasa na huko ni sawa na kuishiwa hoja jambo la msingi watafute takwimu alafu ndipo wazungumze kwa hoja badala ya mihemko"anasema


Shirima anasema baadhi ya vijana walio wengi wamekuwa wakijiingiza katika malumbano ambayo kwa upande wao hawayawezi na kuwa wanapoteza muda badala ya kujishughulisha na mambo yenye msingi kwa maendeleo yao ya baadae.


"Suala la deni la taifa lipo wazi na jinsi litakavyojilipa na hakuna sehemu ambayo unaweza kukopeshwa hela bila kujulikana itarudije hii uliona wapi katika ulimwengu wa sasa"amesema


Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo ni kuwa fedha zilizochukuliwa kama mkopo haziingii mfukoni mwa mtu au watu na badala yake zinaenda kuwekezwa katika miradi ya kimkakati ambayo inajiendesha kwa faida. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS