Header Ads Widget

ULEVI,MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KIKWAZIO CHA MAENDELEO KWA VIJANA...

 

Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP, MOSHI

Vijana walio wengi wametajwa kujihusisha na vitendo vya ulevi uliokithiri sanjari na matumizi ya dawa za kulevya hali inayopelekea wengi wao kudhoofu lakini pia kuishia katika lindi la umaskini uliopitiliza.


Jambo hili linaelezwa sio tu kwa vijana wa Moshi Vijijini bali katika maeneo mengine na kuwa jitihada za maksudi zisipofanyika huenda kundi hili ambalo ndio tegemezi kwa ustawi wa taifa likaishia sehemu mbaya zaidi.


Yuvenail Shirima ni mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)ambapo anasema inasikitisha pale serikali inapopambana kuwainua vijana kupitia fursa mbalimbali lakini wanaotegemewa wenyewe tayari hawapo katika njia sahihi ya kusaidika.


Amesema kuwa ipo haja sasa kundi kuona athari za ulevi huo ambao unakwamisha maendeleo lakini pia unakwamisha mipango mbalimbali ya serikali inayoweka.


"Kinachotukwamisha vijana sasa ni ulevi tena wa matumizi ya dawa za kulevya hii ni aibu kwa taifa na kila kiongozi ana wajibu wa kukemea bila kupepesa macho jambo hili tunaenda kujenga taifa gani?"anahoji Shirima

Shirima anatoa kauli hii katika hafla ya kukabidhi ofisi mpya ya umoja huo kata ya Kirua Vunjo Kusini sambamba na kutekeleza ahadi yake ya kutoa vyombo vya mziki kama sehemu ya kitega uchumi ndani ya umoja huo.


"Niliahidi na nimetekeleza nawashukuru sana kwa moyo wenu ambao mliniamini kama katibu kata wa UVCCM ila nimechaguliwa mwenyekiti wa UVCCM wilaya hivyo nawaomba mniunge mkono"anasema


Anasema kuwa kutokana na ulevi uliokithiri umepelekea vijana wengi kukumbwa na maambukizi mapya ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi hivyo ipo haja kwa kundi hili kuona ulevi sio suluhisho katika ugumu wa maisha wanayopitia na kuwa ulevi hata siku moja haujawahi kumuacha mtu salama.


"Maambukizi ya VVU yanaonyesha asilimia sitini ni vijana sasa haya ndio matokeo ya ulevi hapa tujiulize hii miradi ambayo serikali inayopambania itakuja kumnufaisha nani kama ndio hivi tunakwisha?"anahoji


Proches Njau ni mwenyekiti wa umoja huo kata ya Kirua Vunjo Kusini amesema kwa sasa wanaenda kupiga hatua mpya ya kimaendeleo hususan ya kiuchumi kutokana na kupata ofisi ambayo hapo awali hawakuwa nayo.


"Tumepata ofisi lakini na vyombo vya mziki hii ni ishara kuwa vijana tunaenda kukijenga na kuwa na maoni mapana zaidi katika kujikwamua na wimbi kubwa la umaskini"amesema

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS