NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Mkurugenzi wa kampuni ya Rock Solution Zacharia Nzuki kuwakatia bima watoto takribani 150 waishio mazingira magumu katika vituo vya Hope, Peace of orphanage center na Mvuma Family vilivyopo wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Hayo ameyabainisha baada ya watoto wanaoishi katika vituo hivyo kueleza changamoto zinazowakabili na kueleza kuwa kuwakatia bima hizo zitawasaidia Kwa kiasi kikubwa pindi wanapopata changamoto ya kiafya.
Nzuki amesema kuwa mbali na kutoa misaada mbalimbali, lakini kupitia bima itawasaidia kupata huduma ya kiafya kiurahisi pale wanapopata changamoto.
"Sisi Kama kampuni kupitia hii sherehe hapa kahama tumetoa msaada wa bima ya afya mbali na kutoa misaada mbalimbali lakini msaada mkubwa ni wa kiafya kabla ya kufanya mambo yote Afya kwanza ndio kitu Cha muhimu Kwa jamii" amesema Nzuki.
Amesema kuwa Kama Kuna watu wenye uwezo waweze kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ili na wao waweze kujiona wanastahili kwenye jamii Kwa kuwapa msaada na sio kukaa wao Kwa wao wenye uwezo na kustarehe nao.
" Kampuni yetu ni kubwa tunaamini kwamba tunachokipata sio chetu Kuna watu ambao wanahitaji kusaidiwa, Kwa hali ya kawaida sisi tungekuwa tumeita marafiki zetu tunafurahi nao lakini Leo tupo hali ya chini kabisa kuweza kusheherekea na watoto wanaoishi katika mazingira magumu" amesema Nzuki.
Kwa upande wake mchungaji wa kanisa la Bethel Assembly of God Peter Jonas ameeleza kuwa katika kusherekea sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya watu wengi wamekuwa wakisherekea kinyume na maana nzima ya sherehe hizo na kuacha Msingi na njia ya kweli ya kusudi la sikukuu.
"Lakini kampuni ya Rock Solution wameweza kuwakumbuka watoto Hawa na Kila mmoja anapaswa kuiga Jambo hili zuri linaloweza kumpendeza Mungu" Amesema Jonas.
Baadhi ya watoto wanaoishi katika vituo hivyo wamemshukru Mkurugenzi wa kampuni hiyo Kwa kuweza kuwakatia bima za afya kwani ni Jambo ambalo lilikuwa linawapa changamoto pindi wanapopata changamoto ya kiafya.
" Tunamshukru sana mkurugenzi wa Rock Solution Kwa kuona jambo hili ni muhimu kwetu hatuna Cha kumlipa Ila Mungu pekee ndio atamlipa" Walisema.
0 Comments