Header Ads Widget

PROF NDAKIDEMI ARIDHISHWA KASI UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA....

Na Gift Mongi, MATUKIO,DAIMA APP MOSHI.

Kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali za sekondari jimbo la Moshi Vijijini imetajwa kuridhisha na hivyo kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi atayekwama kujiunga na kidato cha  kwanza mwakani kwa kisingizio cha uhaba wa vyumba vya madarasa.


Haya ndio malengo ya serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kuwa kunakuwepo  na idadi ya kutosha ya vyumba vya madarasa na kuondoa adha ya wanafunzi kushindwa kujiunga na kidato cha kwanza licha ya kufaulu kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali nchini.


Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua vyumba vya madarasa kwenye shule mbalimbali za sekondari mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amesema kasi ya ujenzi huo inaridhisha na kuwa malengo ya serikali yanaenda kutimia kwa kiwango stahiki.

"Kwanza nimshukuru rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutambua na kuona umuhimu wa kuwa na vyumba vya madarasa vyakutosha na uzuri wake hapa kwetu tumefanya kwa kiwango kinachostahili tumefanya kwa kasi na ubora"amesema Prof Ndakidemi


Aidha Prof Ndakidemi amewashukuru viongozi katika ngazi zote waliosimamia zoezi hilo ambalo lina manufaa kwa taifa badala ya kuwaacha wanaofaulu mitaani bila ujuzi wowote ule na kuwa kasi iliyooneshwa ni dhahiri kuwa upo mwamko sasa katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kuleta maendeleo.


Katika hatua nyingine mbunge huyo  amesema baada ya serikali kutimiza wajibu wake ni wakati wa wazazi na walezi kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha watoto wote wanaandikishwa shule hapo januari 2023.


"Kila jambo lina msimamizi serikali imeshatimiza wajibu wake kuhakikisha vyumba vya madarasa vinapatikana sasa ni wajibu Kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wetu waliofaulu wanaenda kujiunga na kidato cha kwanza mapema mwezi januari hapo mwakani"anasema

Hata hivyo Prof Ndakidemi ametumia fursa hiyo kuwatakia wananchi wote heri ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya huku akiwasihi wageni waliokuja kwa ajili ya sikukuu waungane na wenyeji katika kuwezesha miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kwenye maeneo yao.


"Wakikuta mradi ambao unatekelezwa kwa nguvu za wananchi sio mbaya na wao wakaunga mkono maana hapa bado ni nyumbani kwao hawezi kuja mtu kutoka eneo lingine alete maendeleo hapa lazima iwe sisi wenyewe"anasema


Martin Mushi mkazi wa kijiji cha Boro kata ya Kibosho kati amesema miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali na ile ya wahisani ni vyema wananchi nao wakaunga mkono ili iwe endelevu.


"Tunafurahi kuona maendeleo yanakuja huku kwetu lakini sisi wananchi hatuna budi kuunga mkono kwa hali na mali na kuifanya iwe endelevu kwa faida ya vizazi vijavyo"anasema




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI