Header Ads Widget

SHIRIKA LA NDEGE NCHINI MOROCCO LIMETOA SAFARI 30 KWA MASHABIKI WA SOKA KWENDA QATAR

 

Shirika la ndege nchini Morocco, Royal Air Maroc litafanya safari za ndege 30 maalum kwa ajili ya kuwabeba mashabiki wa soka kutoka Casablanca hadi Doha kushuhudia nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Ufaransa mchezo utakaopigwa kesho Jumatano, 14, 2022 huko Qatar.


Ndege hizo zitafanya safari zake kuanzia leo na kesho ambapo abiria watasafiri kwa Bei ya chini ya kwenda na kurudi ili kuongeza idadi ya maelfu ya raia wa Morocco ambao tayari wanahudhuria michuano hiyo mikubwa ya soka huko Doha.


Ikumbukwe kuwa Morocco imeweka historia ya kuwa nchi ya kwanza kutoka Afrika kufika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia tangu ilipoanzishwa mwaka 1930 na watacheza dhidi ya bingwa mtetezi Ufaransa aliyetwaa taji hilo mwaka 2018.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS