Header Ads Widget

MOTO WAUNGUZA MADUKA MATATU

 

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora  Mohamedi Shomari akiwa eneo la tukio wakati wakuzima moto katika barabara ya salimini manispaa ya Tabora

 Shuhuda Katika tukio hilo ambaye ni mfanyabiashara Matata Saidi Matata akizungumza katika  tukio la moto.

watu mbalimbali waliojitokeza kuangalia tukio hilo la moto lililotokea jana asubuhi manispaa ya Tabora .

 wananchi mbalimbali wakiwa jirani na duka lililopata ajali ya moto

                                                   xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Lucas Raphael,Tabora

Moto mkubwa umeteketeza mali mbalimbali za samani za ndani ambazo hadi sasa thamani yake haijaweza kufahamika baada ya Maduka matatu ya wafanyabiashara yaliopo katika barabara ya Salimini Mkoani Tabora

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora  Mohamedi Shomari alisema majira ya 4 na  dakika kumi walipata wito wa  tukio la Moto kwenye fremu za Maduka.

Alisema kwamba Jeshi la Zimamoto  na Uokoaji lilifika kwenye tukio  kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na Usalama , Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi na walifanikiwa kulikabili tukio hilo .

Alisema Maduka matatu yaliteketea kwa moto na Stoo za kuhifadhia mali na baadhi ya samani ziliokolewa .

Kwa Upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora  Richard Abwao alisema kwamba mtu mmoja ambaye ni Mmiliki wa duka mojawapo alipopata taarifa alifika eneo la tukio na alidondoka chini na kupoteza fahamu hivyo alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa Kitete.

Alisema kwamba jeshi la polisi kwa kushirikia na shirika la umeme Tanesco wanaendelea na uchunguzi wa kina kubaini nini chanzo cha moto huo .

Alisema mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo jeshi hilo litatoa taarifa kwa umma na kuwataka wafanyabiashara hao kuwa watulivu katika kipindi hiki cha majonzi.

 

Nae Shuhuda Katika tukio hilo ambaye ni mfanyabiashara Matata Saidi Matata akizungumza katika tukio hilo alisema kwamba  lilitokea ghafla baada ya Mmiliki aliyeunguliwa duka Juma White akiwa ameingia ndani na kukuta tayari moto unawaka.

Alisema muda kidogo alitoka na kuita wafanyabiashara wenzake ili wakamsaidie kuokoa vitu vilivyopo dukani ,Lakini wakamuona anakimbia kuchukua bodaboda na kuelekea Ofisi ya Jeshi la Zima moto na Uokoaji kwenda kutoa taarifa.

Matata ambaye ni Shuhuda anaiomba Serikali kuongeza Magari ya Zima Moto na Uokoaji kwa sababu yangekuwepo mawili au matatu wangefanikiwa kuotoa vitu vingi.

Aidha alisema moto ulikuwa mkubwa ambao ulikuwa umetanda katika duka moja la Juma White ambapo ndio ulianza dukani kwake na kutambaa hadi maduka mengine mawili.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI