Header Ads Widget

MKUUU WA WILAYA MBINGA AGAWA MICHE YA MITI YA MATUNDA KWA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI WA HALMASHAURI YA MJI MBINGA


 Mkuu wa Wilaya Mbinga Aziza Mangosongo amegawa miche ya miti ya matunda kwa watendaji kata na Vijiji wa Halmashauri ya Mji Mbinga, Katika eneo la Kihaha ambako kitalu ya Miche hiyo kimeoteshwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), ambao ndio wasimamizi wa vitalo vya miche mbalimbali ya matunda na Miche ya miti mingine, Zoezi hili ni kampeni ya Kitaifa ya upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ili kukabiliana na athari za ukataji wa miti ovyo, pamoja na uharibifu wa mazingira.


Ambapo awali ya yote Mhe. Mkuu wa Wilaya alitembelea vitalo vya miche ya matunda na alipokea taarifa kutoka kwa Kaimu Meneja wa (TFS), Kuhusu aina ya miche ya miti ya matunda ambayo TFS wameotesha kwenye vitalo hivyo, Aina ya Miche ni Miparachichi, Miembe na Miche ya Machungwa, Hivyo basi Mhe. Mkuu wa Wilaya aligawa Miche ya miti ya matunda zaidi ya 1500 kwa watendaji kata na Vijiji wa Halmashauri ya Mji Mbinga.


Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya Mbinga Aliwataka Watendaji hao kuotesha miche hiyo katika maeneo ya Taasisi wanazoziongoza kwa kushirikiana na Wananchi, Siku ya leo amegawa miche ya miti ya matunda, Lakini mwezi ujao January 2023 itakuwa ni programu maalamu ya kiwilaya ya kupanda miti ya mazao msitu ambapo viongozi na Wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu ili kuendelea kulinda mazingira kwa kuhakikisha upandaji wa miti unakuwa ni zoezi endelevu ili kuepuka athari za ukame na jangwa.


Aidha, Pamoja na mambo mengine Mhe. Mkuu wa Wilaya alisisitiza mambo yafuatayo;


Mosi, Aliwataka Watendaji kata na Vijiji kufuatilia kwa makini ukuaji wa Miche hiyo ili iweze kuleta tija kutokana na juhudi zinazotumika wakati wa upandaji ,Hii ni kutokana na Miche hiyo ikishaoteshwa husaulika na ufuatiliaji wake unakuwa hafifi, hivyo hukauka kutokana na kukosa huduma, Miche hii ifuatiliwe Kama tunavyowafuatilia watoto ili ilete manufaa.


Pili, Aliwataka Watendaji kata na Vijiji kusimamia Sheria za unavaji wa Misitu kwa kushirikiana na TFS, Kupitia zile kamati za Uvunaji wa miti za vijiji ambapo taarifa hizo lazima TFS wazipate, Kwa kufanya hivyo Uvunaji na ukataji hulolela wa Misitu utapungua na Wananchi watafuata Sheria ili uvune msitu lazima upande miti kwanza.


Mwisho Aliwataka Maasifa Misitu wa Halmashauri kuandaa vitalo vya miche mbalimbali katika maeneo yao ili zoezi hili lianzie katika maeneo ya Ofisi za Halmashauri na Miche hiyo igawiwe kwa watumishi ili kuioteshwa katika maeneo tofauti tofauti.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI