Header Ads Widget

MILIONI 107 ZANUNUA VIFAA VYA KUZIMA MOTO NJOMBE

 Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Katika kukabiliana na tatizo la moto unaoteketeza maelfu ya ekari za miti na  kusababisha hasara za mabilioni ya fedha kwa wananchi mkoani Njombe mradi wa pandamiti kibiashara umelazimika kuchukua hatua kwa kuanza kununua vifaa vya kuzima moto  vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 107.


Katika zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo  zikiwemo pikipiki pamoja na kukabidhi muongozo wa sheria ndogondogo za kudhibiti moto  mratibu wa kongani ya Njombe katika mradi wa pandamiti kibiashara bwana Jeremiah Mahendeka amesema mradi huo umeona umuhimu wa kupunguza changamoto ya moto unaoteketeza maelfu ya miti kwa kununua vifaa hivyo kwa ajili ya halmashauri zote za mkoa wa Njombe.


Mshauri mkuu wa mradi huo Michael Hawkes anasema wameona umuhimu wa kutoa vifaa hivyo kutokana na kuripotiwa kwa matukio mengi ya moto ambayo yanakosa vifaa vya kuzima moto na kusababisha hasara kubwa.


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Agnetha Mpangile,Juma Sweda mkuu wa wilaya ya Makete na Lauteri Kanoni Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe wamekiri kuupokea mradi huo na kwenda kusimamia sheria ndogondogo zilizopo pamoja na kuhakikisha mapendekezo ya sheria mpya yanasimamiwa mpaka zinatungwa sheria nyingine.


Akizungumza baada ya kushuhudia makabidhiano ya vifaa hivyo mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema ni lazima hatua stahiki zichukuliwe na mamlaka zote kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya kwa kusimamia sheria na hata kutoa elimu kwa wananchi juu ya sababu zinazosababisha kuzuka kwa moto.


Kwa upande wake Audatus Kashamakula Mhifadhi misitu wilaya ya Njombe na Kaimu Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Njombe Inspector Joel Mwakanyasa wametaka vifaa hivyo vikatumike kwa kadri ya malengo.

Moto umekuwa kikwazo kwa wakulima wa misitu mkoani njombe










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS