Header Ads Widget

MANISPAA MTWARA MIKINDANI YATOA MILIONI 244 MIKOPO

 


Zaidi ya shilingi Milioni 244 zimetengwa na Manispaa ya Mtwara Mikindani kwaajil ya mikopo ya  vikundi zaidi ya 34 vya wanawake 24 vijana 4 walemavu 7.


Akizungumza katika mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa kwaajili ya vikundi hivyo kupata mikopo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Juliana Manyama amevitaka vikundi vya wanawake, vijana na walemavu wanapatiwa mafunzo kwaajli ya mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri kuzingatia mafunzo hayo ili kuhakikisha kuwa lengo la serikali kusaidia vikundi hivyo linatekelezeka.


“Tumetoa mafunzo ya siku tano ya vikundi 35 vitakavyopatiwa mkopo na halmashauir hiyo baada ya kupita baada ya mchujo wa vikundi 74 vilivyowasilisha maombi ya mikopo ya asilimia 10  inayotengwa kwaajili ya makundi ya wanawake vijana na walemavu.


“Tunatoa mafunzo hayo kwa siku tano vikundi hivyo  vikiiva tutawapa pesa hizo ambapo tunawafundisha  ujasiliamali, utunzaji wa fedha, uongozi namna bora ya kuongoza na kuwajenga ili wawe wafanyebiashara kwa tija”



“Sisi huwa hatutoi mikopo bila mafunzo tunawajengea uwezo na kuwaambia fursa zilizopo ili waweze kunufaika nazo ikiwemo kupata mikopo mbalimbali tofauti nah ii tunayotoa sisi kwakuwa wanauwezo” alisema Manyama


Nae Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Mtwara Mikindani Lida Kaungenge Lengo ni kuwajengea uwezo juu ya matumizi ya fedha wanazokopeshwa.


elimu hiyo inatolewa kulingana na malengo na  kanuni ambazo zimeelekezwa kwa kikundi kitakacho kiuka na kufanya malengo ambayo hayajakusudiwa watachukuliwa hatua vilikuja vikundi 74 vililoeta maombi vikundi 35 vilikidhi vigezo hii tunaangalia shughuli wanazoenda kufanya”  alisema Kaungenge


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI