Header Ads Widget

WAKAZI WA NAMTUMBO WATAKIWA KUTAMBUA KAZI ZINAZOFANYWA NA MANTRA PAMOJA NA SERIKALI

  


    

Na Amon Mtega, Namtumbo.


WAKAZI wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma wametakiwa kutambua kazi mbalimbali zinazofanywa kwenye jamii na kampuni ya Mantra Tanzania Limited pamoja na Serikali ili jamii iendelee kunufaika na kazi hizo.


Wito huo umetolewa na Afisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Peres Kamugisha wakati wa uzinduzi wa maktaba ya kisasa iliyofanywa na kampuni ya Mantra katika shule ya Sekondari ya Msindo iliyogharimu zaidi ya sh.Milioni 32  kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kujiongezea maarifa katika masomo yao.


Kamgisha ambaye amekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Namtumbo Chiriku Chilumba amesema kuwa kampuni ya Mantra inayojishughulisha na madini ya urani kwenye Wilaya hiyo imekuwa ikifanya kazi mbalimbali za maendeleo kwenye jamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya Wilaya ya Namtumbo kwa kushirikiana na Serikali na kuifanya jamii iweze kusongambele hivyo ni vema kazi hizo zikaungwa mkono.



 Awali akitoa taarifa ya uwepo wa maktaba hiyo mkurugenzi mwenza wa kampuni inayoshughulika na mambo ya ukarabati ya Realizing Education for Development (READ)Lusebelo Mwalughelo amesema kuwa katika uwekaji wa maktaba hiyo kazi mbalimbali zimefanywa ikiwemo kulikarabati darasa moja ili litumike kwa maktaba umetumika ukarabati mkubwa ikiwemo na kuviweka vifaa vya kimaktaba.



Mwalughelo amesema kuwa kampuni ya Read ambayo ilipewa kazi na kampuni ya Mantra ya kuhakikisha maktaba hiyo inakuwa ya kisasa ili kuendana na teknolojia ya sasa imeweka vifaa ambavyo ni Vitabu zaidi ya 700 ambavyo vimezingatia mahitaji ya wanafunzi,Compyuta nne meza na viti.


Naye mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Getrudi Mwakalobo amesema kuwa kuwepo kwa maktaba hiyo itawafanya wanafunzi hao kuzidi kuongeza ufaulu katika masomo yao kwa kuwa miundombinu ya kielimu imeshakamilika.


Pia mkuu wa Shule hiyo Henry Milanzi akiishukuru kampuni ya Mantra amesema kuwa ilikuwa ni ndoto ya siku nyingi na sasa imetimia na kuwa wanafunzi wake anategemea wataongeza uelewa zaidi tofauti na misimu ya nyuma.



 Hata hivyo meneja uhusiano wa kampuni ya Mantra Khadija Kawawa amesema kuwa kampuni hiyo licha ya kufanya kazi mbalimbali kwenye jamii lakini imeshaweka maktaba katika shule nane za Sekondari kwenye Wilaya hiyo .


Khadija amefafanua kuwa kazi hizo zinazofanywa na kampuni hiyo ni sehemu ya kuungamkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambayo inafanya kazi katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya shule hapa Nchini.



        

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI