Header Ads Widget

MAMIA WAJITOKEZA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU KATA WA CCM..

Na Gift Mongi, MATUKIO DAIMA APP, MOSHI

Mamia ya wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) leo Desemba 20.2022 wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa katibu wa chama cha mapinduzi(CCM)kata ya Kilema kati katika jimbo la Vunjo  Sebastian Mosha.


Wanachama hao wakiongozwa na katibu  wa CCM Mkoa Jonathan Mabihya wamemwelezea marehemu kuwa ni mtu aliyejitoa kwa hali na mali katika kukitumikia chama.


"Marehemu alitumia muda wake enzi za uhai wake katika kukijenga chama hivyo ameacha alama katika eneo alilokuwa analiongoza kwa kweli huu ni mfano wakuigwa"amesema   


Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima amesema marehemu atakumbukwa kutokana na umahiri wake katika kuwaunganisha wanachama.


"Marehemu aliwaunganisha wanachama Kwa njia mbali mbali na leo  hii tuko hapa kumuaga na kumuweka katika nyumba yake ya milele ni vyema tukabaki na yale mema aliyotufundisha"amesema


Aidha Shirima amesema wakati huu ambapo chama kimempoteza mtu makini ni vizuri kwa pamoja kuungana na kuendelea kutenda yale mema aliyoyaamini enzi za uhai wake.


Kwa upande mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya wa chama cha mapinduzi wilaya ya Moshi Vijijini Emmanuel Mlaki ameungana na wanachama wengine kutoa pole kufuatia msiba huo na kuwataka wanachama kumuombea kwa Mungu marehemu.


Amesema kila jambo linalofanyika lina sababu mbele za Mungu hivyo hata tukio lililotokea ni mipango yake na badala ya kuendelea kusikitika ni bora kumuombea katika makazi yake hayo mapya.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI