Header Ads Widget

KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA BALOZI MUSHY.....

Na Gift Mongi,MATUKIO DAIMA APP, Moshi. 

Aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Austria Celestine Mushy amezikwa  kijijini kwao eneo la Kibosho road huku rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wakiongoza shughuli hiyo ya mazishi.


Desemba 13 mwaka huu ndipo balozi Mushy alipoteza maisha katika eneo la Mkata wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambapo gari alilokuwa akisafiria liligongana na lori la mizigo na kuungua moto akiwa ndani.


Kama tukio lilivyogusa hisia za watu wengi  viongozi mbalimbali wa dini pamoja na ndugu jamaa na mafariki wamefika nyumbani hapo kwa ajili ya kumsindikiza katika makazi yake ya milele


Taarifa kutoka wenye familia zinaeleza Balozi Mushy  ameacha watoto wawili na mke aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari 2022 na Mei 5, 2022 akawasilisha hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.


Akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mazishi hayo, Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka amesema chama hicho kitamkumbuka Balozi Mushy kama nyenzo kuu ya mchango wa maendeleo katika taifa.


"Tuamepata pigo sio kama chama pekee Bali hata serikali na taifa kwa ujumla baada ya kuondokewa na mtu kama huyu ambaye alikuwa shupavu katika kupigania kile alichokiamini kina maslahi"alisema na kuongeza 


"Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa hasa katika mchango mkubwa wa Balozi Mushy katika kuimarisha na kuelimisha ushirikiano wa kimataifa hivyo chama kinathamini mchango wake alioutoa,


Alisema watumishi wengine waliobakia wamesikia Balozi Mushy akizungumziwa wema na mazuri lakini alama aliyoiacha        Balozi Mushy katika maeneo aliyofanya kazi. 


"Ni matumaini yetu mwenzetu ametangulia lakini funzo kwetu kubwa ambalo tumepata nyuma yake ni kwamba tupande na tuweke alama na mbegu ya wema," alisema Shaka

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI