NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewataka viongozi wa machinga kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaofanya biashara kinyume na sheria na taratibu katika maeneo yasiyo rasmi.
Ameyasema hayo wakati wa kikao Cha kamati ya ushauri ( RCC) kilichofanyika Jana Mkoani hapa na kueleza kuwa machinga wote wanapaswa kurudi kwenye maeneo yao waliopangiwa toka awali na kuacha kufanya biashara katika maeneo ambayo sio rasmi na rafiki kwao.
Malima ameeleza kuwa mji wa Mwanza unapaswa kuwa wa kitalii na wa kisasa endapo machinga wataendelea kufanya biashara zao kiholela bila mpangilio na kuacha maeneo rasmi waliopangiwa hauwezi kuwa Tena kama wanavyotaka uwe.
"Mimi nimekaa London Kwa muda mrefu na huko pia Kuna machinga wa aina zote lakini wanafuata taratibu walizopangiwa na siku ya ratiba yao wanafungua mitaa ili machinga wafanye biashara zao iweje huku hawataki kukaa katika maeneo yao" Alisema Malima.
Amewataka viongozi wa pande zote mbili kwenda kuzungumza na wafanyabiashara hao waondoke katika maneno hayo na kama Kuna tatizo lolote wanapaswa kwenda kumuona Mkuu wa Mkoa mwenyewe ili aweze kuwatatulia shida zao na sio kujichukulia wao sheria ya kwenda kufanya biashara katika maeneo ambayo sio rasmi.
"Nendeni mkazungumze na watu wenu maana wanawasikiliza ninyi na sitaki wafanye fujo ndani ya Mkoa wangu na mkifanya fujo tutaonana na nyie viongozi Tena wa pande zote mbili" Alisema Malima.
Hata hivyo ametoa wito Kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mkurugenzi wa Jiji kuhakikisha wanatengeneza miundombinu rafiki katika maeneo yote rasmi waliyoyachagua Kwa ajili ya wafanyabiashara hao kufanyia biashara zao
0 Comments