Afisa Kilimo kata ya Pangale na Mwezeshaji wa walengwa wa Tasaf Josephine Mzoo wakati wa uhawilishaji uliofanyika katika kijiji cha kipanga mlimani akizungumza na walengwa hao .
Walengwa wa Tasaf katika kjiji cha Kipanga mlimani na kata ya Kipanga wapo nje ya ofisi ya mtendaji wa kijiji cha kipanga mlimani wakisubiri kupatiwa fedha ..
Afisa Kilimo kata ya Pangale na Mwezeshaji wa Tasaf Josephine Mzoo akifanya uhawilishaji kwa mmoja ya walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini Tasaf .
Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini Tasaf katika kjiji cha kipanga Mlimani wakimsikiliza mwezeshaji wa Tasaf hayupo pichani .
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Lucas Raphael,Tabora
Walengwa wa Tasaf wilayani sikonge mkoani Tabora wameshauriwa kulima mazao yanayo stahimili ukame kulingana na kuwepo kwa mvua kidogo inayotarajia kunyehesha msimu huu wa kilimo.
Wito huo umetolewa jana na Afisa Kilimo kata ya Pangale na Mwezeshaji wa walengwa wa Tasaf Josephine Mzoo wakati wa uhawilishaji uliofanyika katika kijiji cha kipanga kata ya kipanga Mlimani wilayani Sikonge mkoani hapo.
Alisema kwamba wakulima wanapaswa kulima mazao kinga njaa ambayo ni Viazi na Mihogo ili kuweza kukabiliana na njaa inayoweza kujitokeza katika msimu wa kilimo mwaka huu .
Josephine aliendelea kusema kwamba mvua za mwaka huu ni chache kulingana na utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa mvua zitanyesha chini ya wastani.
Naye mlengwa wa Tasaf katika kjiji cha Kipanga mlimani na kata ya Kipanga Nelea Katumbo alisema kwamba watajitahidi kulima mazao yanayostahimili ukame ili kuweza kupata chakula katika msimu huu wa kilimo .
Alisema kwamba licha ya kulima mazao hayo pia amefanikiwa kufuga kuku na kisha kuweza kununua mbuzi na sasa ana mbuzi 11 ambao ana lengo la kuuza na kununua Ng’ombe .
Alisema kwamba toka kujiunga na mfuko huo amefanikiwa kimaisha kwa kuweza kujihudumia kwa chakula, kuweza kumudu kulima mazao mbalimbali kwa pesa anayopata, anatoa pesa nyingine kwa ajili ya mahitaji ya wanafunzi na chakula inayobaki kwa ajili ya mbolea kwa ajili ya shamba .
Alisema kwamba licha ya kutumia mbolea ya samadi kwenye mashamba lakini pia anatumia mbole ya madukani kwa ajili ya kupata mazao bora.
Naye Zafarani Hussein alisema kwamba kulingana na utabiri wa hali ya hewa unaosema mvua za mwaka huu zitanyesha chini ya wastani jambo ambalo wanalazimika kulima mazao yanayostahimili ukame.
Alisema ushauri huo ulitolewa na afisa kilimo wanauchukuwa kwa jicho la Tatu kutokana na mvua kunyesha kwa kiwango kidogo ila watajitahidi kuyatunza mazao ambayo tayari wameyapanda .
Hata hivyo amekiri kunufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini – Tasaf kwa kuweza kusomesha watoto, kuanzisha miradi kufuga mbuzi, kuku, bata na Ngombe.
Alisema kuwa tangu ajiunge na TASAF ambapo kwa mwaka huu ameweza kulima na anatarajia kupata gunia 8 za mahindi, lengo ni kuongeza kulima mazao ya kilimo hasa Karanga, Muhogo na kuongeza idadi ya kutoka mbuzi 10 hadi kununua Ng’ombe wa 3 kwa ajili ya kumsaidia kulima mashamba yake .
Alisema kwamba licha ya kununua Ng’ombe hao pia amenunua jembe la kukokotwa na Ng’ombe kitu ambacho kitamsaidia kulima mashamba makubwa kikubwa kuona mvua inayesha vizuri .
“Tunaishukuru sana serikali kwa kutuondolea umaskini huku vijijini kwetu, kama sio fedha hizo mimi ningekuwa nimeshakufa, lakini kutokana na fedha hizo zimenisaida kimaendeleo”alisema Zafarani Husein
Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya Jamii wilaya ya sikonge’ Claud Nkanwa Alisema walengwa wameendelea kupewa mafunzo ya kujiwekeza katika rasilimali zalishi ili pindi mpango huo utakapoisha au kipindi chao kitakapoisha waweze kujiwezesha kuendelea na Maisha yaliyo bora .
Hata hivyo aliwataka wananchi wanaonufaika na mpango huo wa kunusuru kaya masikini TASAF kuzitumia fedha hizo kama ambavyo wamekuwa wakifundishwa na viongozi wa TASAF huku akisema yeye atakuwa mfuatiliaji wa fedha hizo.
0 Comments