Waziri wa
Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati alipozungumza
na wananchi wa Kyela (hawapo pichani) katika hafla ya utiaji saini wa mkataba
wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira
Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi (KM 4), mkoani Mbeya.
Mbunge wa Kyela Mhe. Ali Mlagila Jumbe akisisitiza jambo katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi Port (KM 4), uliosainiwa katika Viwanja vya shule ya msingi Mpanda, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya mara baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi (KM 4), Uliosaniwa katika Viwanjavya shule ya Msingi Mpanda, wilayani Kyela, mkoani Mbeya.
Sehemu ya wanachi wa Wilayani Kyela wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa( hayupo pichani) wakati alipozungumza nao katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi Port (KM 4), katika viwanja vya shule ya msingi Mpanda, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila (Kulia) na Muwakilishi wa Kampuni ya AVM-Dilingham Construction International Incorporated ya Nchini Uturuki mara baada ya kusaini Mkataba kwa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi Port (KM 4), uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mpanda, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya.
Waziri wa
Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia waliokaa) katika picha
ya pamoja na Viongozi wa Wizara, Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Kyela Wakala wa
Barabara Nchini (TANROADS) mara baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele
(KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi (KM 4),
uliosaniwa Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.
(PICHA NA
WUU)
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Serikali
imesema itaendelea kutekeleza Sera yake ya kuunganisha mkoa kwa mkoa na wilaya
kwa wilaya kwa barabara za lami ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria,
mazao na malighafi mbalimbali ili kukuza uchumi kwa haraka.
Akizungumza
wilayani Kyela wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda
hadi Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele
hadi Itungi Port (KM 4) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kukamilika kwa barabara hizo
kutaimarisha shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa wilaya za Rungwe na Kyela, na mikoa
ya Ruvuma, Njombe na nchi jirani ya Malawi.
“Katika
ukanda huu kuna malighafi na mazao ya kilimo,uvuvi na makaa ya mawe mengi yanayohitaji
miundombinu rafiki kwa ajili ya kuwafikia watumiaji kwa wakati, ndio maana
Serikali ya awamu ya sita imeamua kujenga barabara hizi kwa pamoja,’ amesema
Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof.
Mbarawa amewataka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kumsimamia vizuri Mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili azingatie
viwango na thamani ya fedha kulingana na
mikataba.
Aidha,
Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Kyela kuwa TANROADS
itafanya uthamini upya ili kuhakikisha wananchi wanaopisha ujenzi wa barabara
hizo wanapata stahili zao kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande
wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema Kampuni ya AVM
Dillingham Construction International Incorporated ya Nchini Uturuki imeshinda
zabuni ya kujenga barabara hiyo na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24
kuanzia sasa.
Zaidi ya
shilingi bilioni 38 fedha za ndani zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo
ambao pia utahusisha taa za barabarani.
Mkuu wa mkoa
wa Mbeya juma homera amewataka wananchi wa kyela kutumia fursa za ajira
zitakazojitokeza wakati wa mradi huo kufanyakazi kwa bidii na uzalendo ili
kuwezesha maradi huo kukamilika kwa wakati.
Kwa upande
wake Mbunge wa ileje ambae pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi mhandisi Godfrey
Kasekenya amesema ujenzi wa barabara wilayani kyela ni muendelezo wa mkakati wa
serikali katika kuhakikisha barabara zote za nyanda za juu kusini zinazopiyta
maeneo ya uzalishaji zinakuwa katika viwango bora na hivyo kutumika wakati wote
na kuongeza tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
(Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi)
0 Comments