Header Ads Widget

ABIRIA 57 WANUSURIKA KIFO MKOANI MOROGORO

Abiria 57 waliokuwa wakisafiri na basi la Al Saedy wamenusurika kifo baada ya basi hilo kupinduka wakati dereva wa basi hilo akikwepa kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ally's katika eneo la Kitungwa Kingolwira Manispaa ya Morogoro.


Ajali hiyo imetokea leo Jumatano Desemba 28 asubuhi katika barabara kuu ya Pwani-Morogoro na kusababisha abiria 16 kupata majeraha madogo ambao walipatiwa huduma ya kwanza na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoji huku kondakta wa basi hilo akikipelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.


Akizungumza katika eneo la tukio, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Morogoro, Sauda Mohamed amesema basi hilo lilikuwa likitokea wilayani Kilosa kwenda Dar es Salaam na ilipofika eneo la Kitungwa lilipinduka.


Mohamed amesema baada ya kutokea kwa ajali hiyo askari wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walifika eneo hilo na kutoa huduma ya kwanza kwa abiria ambao wamepata majeraha madogo madogo pia  walifanya jitihada ya kuwasiliana na uongozi wa basi la Al Saedy ili kupata basi lingine abiria waweze kuendelea na safari yao.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro, Emmanuel Ochieng amesema askari wa jeshi hilo walifika kwa wakati eneo la tukio na kutoa huduma ya kwanza kwa abiria 16 ambao wamepata majeraha mepesi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI