Katika kuimarisha uhusiano na
ujirani mwema, kampuni ya Mantra Tanzania Limited inayomiliki
mradi wa madini ya Urani wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, imekabidhi jenereta
na jokofu vyenye thamani ya zaidi ya Tshs. Millioni 25 kwa wafanyakazi wa
hifadhi ya Taifa ya Nyerere kanda ya Likuyusekamaganga iliyopo wilayani humo.
Akizungumza katika makabidhiano
hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania Ndugu Alexander Ryabchenko amesema
kuwa, tukio hili ni ishara ya ujirani mwema kwani kampuni hii haitazamii kuwa
na mahusiano mazuri tu na jamii inayozunguka mradi, lakini pia na taasisi za
serikali na binafsi ambazo kwa namna moja au nyingine ni wadau muhimu wa
kampuni hiyo na wilaya nzima ya Namtumbo.
Vilevile ndugu Beria Voster
ambaye ni Msimamizi wa Mradi huo wa urani, ametoa shukrani za dhati kwa
wahifadhi kwani wamekuwa wakionesha ushirikiano wa pekee kwa kampuni ya Mantra
Tanzania na kuhimiza kudumisha ushirikiano huu baina ya taasisi hizo mbili
kwani wote wana nia njema ya kujenga na kuchangia ukuaji wa uchumi katika taifa
letu.
“Huu si mwisho bali ni mwanzo
mzuri wa ushirikiano wetu endelevu, tukio hili ni ishara ya shukrani kutoka kwa
kampuni ya Mantra kwani mara zote TANAPA kupitia hifadhi hii ya Nyerere imekuwa
msaada mkubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo ulinzi dhidi ya wanyama wakati
shughuli za mradi zinapoelekea katika hatua za mwanzo za uchimbaji” Alisema
Ndugu Voster.
Nae Ndugu Shangwe Kakulu kwa
niamba ya wafanyakazi wenzake wa TANAPA waliopo katika hifadhi ya Nyerere kanda
ya Likuyusekamaganga ametoa shukrani za dhati na kusisitiza kuwa ushirikiano
huo baina yao na kampuni ya Mantra utazidi kuwa endelevu kwani mbali na
majukumu ya kazi, taasisi hizo zimekuwa marafiki wazuri pamoja na taasisi
zingine ambazo ni wadau wa TANAPA. Bwana Kakulu alisisitiza kuwa, ushirikiano
huo utaendelezwa baina ya pande zote mbili ili jamii izidi kunufaika kutokana
na uwepo wa taasisi hiyo ya uhifadhi na mradi huo wa Mantra.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya
Mantra Tanzania Bi. Khadija Kawawa amesema kuwa mbali na kufanya majukumu ya
kijamii ambayo Mantra hujihusisha nayo mara kwa mara, kampuni ya Mantra inatazamia
kuendeleza ushirikiano kwa wadau wake wa karibu na muhimu kama ilivyofanya kwa
wafanyakazi hao wa hifadhi ya Nyerere wa kanda ya Likuyusekamaganga. “Hii ni
ishara sio ushirikiano tu, bali upendo ambao kampuni ya Mantra inao kwa wadau
wote wa maendeleo waliopo wilayani Namtumbo na Ruvuma kwa ujumla.
Kwa upande wa watumishi hao wa
hifadhi ya Nyerere kanda ya Likuyusekamaganga wameishukuru kampuni ya Mantra
kwa kuwa ushirikiano na kuahidi kuudumisha huku ikiendelea kutekeleza majukumu
yake ya msingi ya kuhudumia na kulinda hifadhi hiyo ya taifa.
Ndugu Shangwe Kakulu akizungumza kwa niaba ya
wafanyakazi wa hifadhi ya Nyerere kanza ya Likuyusekamaganga katika kupokea jokofu
na jenereta kama ishara ya ushirikiano baina ya wahifadhi hao na Mantra
Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mantra, Alexander
Ryabchenko akizungumza wakati wa makabidhiano ya jenereta na jokofu kwa
wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere kanda ya Likuyusekamaganga.
Ndugu Shangwe Kalulu akionesha uongozi wa Mantra eneo ambalo
watahifadhi jenereta lililokabidhiwa na kampuni ya Mantra Tanzania Limited
Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra akioneshwa eneo ambapo
jokofu litapowekwa na kuhudumia wafanyakazi wa hifadhi
Msimamizi wa Mradi wa Mantra Tanzania Limited Ndugu Beria Voster akizungumza kutoa shukrani kwa wafanyakazi wa hifadhi ya Nyerere kwa ushirikiano wana zidi kuuonyesha kadri mradi unavyoendelea
0 Comments