Header Ads Widget

ELIMU YA UTUNZAJI WA MISITU YAHITAJIKA KWA JAMII INAYOZUNGUKA MAENEO HAYO.

 

Maafisa misitu mkoani kilimanjaro wameshauriwa kuelekeza macho Yao kwa wananchi katika kutoa elimu ya juu ya umuhimu wa utunzaji wa misitu, kwani imeonekana kuwa misitu inaharibiwa na wananchi wasiokuwa na uelewa wa jinsi ya kutunza misitu.


Hayo yameelezwa na  Abel Musoka Mwanafunzi  wa Stashahada ya teknolojia  ya viwanda katika   chuo Cha viwanda vya misitu  (FITI)  wakati alipokuwa kwenye mdahalo  wa kujadili  juu ya umuhimu wa jamii katika uhifadhi wa misitu uliyofanyika chuoni hapo.


Amesema Kuwa kutokana na uharibifu wa misitu unaoendelea hapa chini kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya tabia ya nchi na kusema kuwa Kama jamii itapewa elimu itasaidia kupunguza tatizo hilo.


"Mabadiliko ya tabia ya nchi kama ukame ,na ukiangalia kwa hapa Kilimanjaro joto limezidi sana na sio hapa tu ni kwa nchi nzima na hii imesababishwa na uvunaji holela wa miti na uharibifu wa mazingira"Alisema.


Hata hivyo ameendelea kusema kuwa Kama misitu ikiharibiwa wanyama ambao wamekuwa vivutio kwa watalii waliopo ndani ya misitu nao wanapotea na wengine kuangamia .


Akizungumza katika mdahalo huo Joseph mjole amesema kuwa Kuna baadhi ya wanajamii wamekuwa wakiharibu misitu kwa kujua lakini wengine wamekuwa wakifanya uharibifu bila ya kuwa na uelewa .


"Na ndio maana kumewekwa Sheria na taratibu ili kuwawajibisha wale wote ambao wanaenda kinyume na taratibu hizo kwa kujua lakini pia ndio maana kunatolewa elimu ili watu wafahamu umuhimu wa utunzaji wa misitu "Alisema Joseph.


kwa upande wake Joseph John Mwanafunzi wa Stashahada ya teknolojia ya viwanda vya misitu amesema kuwa kadri siku zinavyokwenda maeneo ya misitu yanazidi kupungua kwani uvamizi wa wanakijiji katika maeneo ya misitu unazidi kuongezeka .


Amesema jamii inapaswa kutunza na kulinda mipaka kwa ajili ya manufaa endelevu na malighafi zinazotokana na misitu.


Pia ameitaka  jamii kuacha kufanya shughili mbalimbali za kijamii katika vyanzo vinavyozunguka hifadhi za misitu ,kama uchomaji wa mkaa na uvunaji holela wa miti ,pamoja na kulima .


Hata hivyo wanajamii wanashauriwa kupanda miti kwa kuziba mapengo ya miti iliyoharibika mstuni na inayoendana  na Ile iliyovunwa  kwa maana kwamba Kuna miti ambayo imeharibika msituni.


Hata hivyo Serikali kupitia sera  misitu ya mwaka 1998  inasema wanajamii au Wana Kijiji wanashauriwa kuanzishwa vitalu vya miti katika mashamba  Yao.


Akihitimisha mdahalo huo Yona Chilongolo Mkufunzi wa chuo hicho amesema kuwa Kuna umuhimu wa utunzaji wa mazingira na misitu kwani inasaidi ufugaji  wa nyuki ambao wanazalisha asali .


Sambamba na hayo amesema kuwa pia  nyuki wanahusika katika utunzaji wa mazingira kwani wanachavusha baadhi ya mimea na kusema Kama nyuki hawatakuwepo Kuna baadhi ya mimea hayatachavushwa vyema hata kama mkulima ataweka mbolea kiasi gani .


"Jamii ikijikita katika kutunza mazingira Kuna viumbe ambavyo vitaendelea kuwepo kwani viumbe na binadamu tunategemeana"Alisema




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS