Header Ads Widget

DCEA YATOA ONYO KWA WASANII, WASHIRIKA WA CAMBIASSO WAONGEZEKA

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) imesema haitamvumilia mtu yoyote anaehamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo wasanii wanaotunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa hizo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa DCEA General Kusaya wakati alipokuwa akitoa taarifa ya muendelezo wa Oparesheni zilizopita za kuwakamata watu wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambapo amesema DCEA inaendelea kuwasaka wote wanaojihusisha na matumizi ya dawa hizo.


Aidha, amesema kutokana na kuimarika kwa udhibiti wa dawa za kulevya nchini Tanzania wahalifu wa dawa za kulevya wamekua wakibuni mbinu mbalimbali Ili kufanikisha uhalifu hao ambapo mamlaka ipo macho kukabiliana na mabadiliko ya mbinu hizo.


Katika hatua nyengine DCEA imefanikiwa kukamata jumla ya kilo 16.643 za dawa ya kulevya huku ikiwashikilia watuhumiwa saba ambapo  kilo 15 .19 aina ya Heroine ziliwahusisha watuhumiwa watatu ambao ni washirika Kambi Zuberi Seif (CAMBIASSO) na wenzake wakiwa na kilo 34.89 za Heroin.


"Watuhumiwa hawa watatu ni Suleiman Thabit Ngulangwa (36) mfanyabiashara na mkazi wa Salasala, Sharifa Seleman Bakar (41) mkazi wa Maji Matitu - Mbagala na Farid Khamis Said (22) mkazi wa Maji Matitu - Mbagala wote ni wakazi wa Dar es Salaam "amesema Kamishna Kusaya.


Aidha, amesema kuwa watuhumiwa wengine wanne walikamatwa wakiwa na gramu 655.75 za cocaine na gramu 968.67 za Methamphetamine ambapo walikuwa katika harakati za kusafirisha dawa hizo za kulevya kwenda nje ya nchi.


"Watuhumiwa wengine ni Hussein Rajab Mtitu(28) maarufu Chodri   Mohamed mfanyabiashara na mkazi wa Kibonde Maji, Jaalina Rajab Chuma (31) maarufu Jaalina Mohan mjasiriamali na mkazi wa Tandika, Shabani Abdalla Said (36) mkazi wa kilimahewa, Tandika na Iren Dickson Mseluka (39) mkazi wa Ndala Shinyanga"amesema Kamishna Kusaya.


Aidha, amesema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kiupelelezi kukamilika, huku DCEA ikiahidi kushirikiana na makampuni ya usafirishaji wa vifurishi  na wadau wengine katika kudhibiti mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI