Bodi ya Wakurugenzi EWURA, leo Desemba 20, 2022, imefanya ziara ya kikazi katika miundombinu ya kuhifadhia mafuta ya TIPER (Tanzania International Petroleum Reserves Ltd) iliyopo eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, ili kujionea kazi, maendeleo na changamoto mbalimbali inayoikabili kampuni hiyo katika uhifadhi wa mafuta.
Akitoa neno la utangulizi, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya, alisema, EWURA kama mdhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, imefanya ziara hiyo ili kufahamu kiundani utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya uhifadhi wa mafuta nchini, kujua mafanikio na changamoto mbalimbali, ili EWURA iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na tija kwa taifa kwa ujumla.
Aidha, akifanya wasilisho juu ya Utendaji wa Kampuni hiyo, Kaimu Meneja wa TIPER, Bw. Martin Mosha alisema:”TIPER ipo kimkakati ili kuhakikisha nchi inakua na hifadhi ya mafuta ya kutosha kwa matumizi ya nchini na baadhi ya nchi zinazotegemea kupitisha mafuta nchini kama vile Zambia, Kongo, Malawi, Burundi”
Kwasasa TIPER ina ukubwa wa eneo wenye Hekta 58 na maghala 32 yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 253 za mafuta, ikiwa zimeongezeka kutoka lita milioni 140 ilivyokua hapo wakati inaanza kazi.
0 Comments