Header Ads Widget

AWESO ASISITIZA MAHUSIANO MAZURI KATI YA WAKURUGENZI WA MAJI NA WAKUU WA VITENGO VYA UNUNUZI NA UGAVI

 




Teddy Kilanga,Arusha


Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amewataka wakuu wa vitengo vya ununuzi na ugavi  pamoja na wakurugenzi watendaji wa mamlaka za maji nchini kuwa na mahusiano mazuri katika maeneo ya  kazi ili kuziheshimisha taasisi zao na serikali.


Akizungumza katika kikao kazi cha wakuu wa vitengo vya ununuzi na ugavi kilicho chini ya wizara ya maji na Taasisi zake kilichofanyikia jijini Arusha Aweso alisema kumekuwa na migongano ya kimaslahi kwa baadhi ya wakurugenzi watendaji wa maji na wakuu wa vitengo vya ununuzi na ugavi hali ambayo haina afya katika utendaji kazi.


"Tumeona migongano ya kimaslahi ya  kutoelewana kati ya wakurugenzi na wakuu wa ununuzi na ugavi na hata kujaribu kuchafuana kwenye mitandao lakini ni vyema mkakubali kulinda heshima ya taasisi zenu na serikali kwa ujumla,"alisema Aweso.


Aweso alilisisiti wakuu kuboresha mahusiano mahali pa kazi ili kuepusha migongano hiyo isiyo ya lazima katika wizara yake kwani kwa kufanya hivyo anayeumia ni wapokea huduma ambao ni wananchi.


Kamishna wa sera za ununuzi wa umma wa wizara ya fedha na mipango,Dk.Frederick Mwakibinga alisema pamoja na sekta ya maji kufanya vizuri bado kunamalalamiko wanayapata kutoka katika sekta hiyo hivyo ni vyema wakaongeza juhudi katika kuondoa kero za watumiaji.



Naye Katibu mtendaji msaidizi wa mamlaka za rufaa ya zabuni za umma (PPAA)Florida Mapunda alisema wamekuwa wadau katika sekta ya ununuzi wa umma hususani kwenyw miradi ya maji.


"Katika kipindia hiki za miaka miwili hadi mitatu iliyopita malalamiko na migogoro inayotokana na manunuzi ya umma imepungua na mingine imeisha  kwa kiasi kikubwa na wataalamu wamekuwa wakishinda kesi hizo,"alisema Mapunda.


Kwa upande wake mwenyekiti wa wakurugenzi watendaji wa mamlaka za maji ,tanzania Patrick Nzamba alisema katika sekta hiyo bado wanakabiliwa na suala la maadili hivyo wanahitaji kuboresha na kuhimarisha sekta ya maji nchini ingawa wamekuwa wakipewa mafunzo mbalimbali.


"Vilevile bado wanakabiliwa na changamoto katika kuhakikisha wanasimamia mikataba na hii wakati mwingine imepelekea mvutano hivyo wanaishukuru wizara ya maji kwa kutoa msaada wa kutatua changamoto hizo pindi zinapotokea,"alisema Nzamba.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI