Header Ads Widget

ZAINABU MWAMWINDI MWENYEKITI UWT MKOA WA IRINGA,Mhandisi REMBO, MSANII HALIMA NA JANE MWALEMBE WAULA

 


Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa  Iringa wamchagua Kwa kura 198 Zainabu Mwamwindi kuwa mwenyekiti kuwa mwenyekiti mpya wa UWT mkoa wa Iringa huku aliyekuwa Mwenyekiti Nicolina Lulandala akiambulia kura 82.

Akitangaza Matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Ukumbi wa CCM wilaya ya Iringa mjini msimamizi wa uchaguzi huo Peresi Magili alisema kuwa mgombea wa Tatu alikuwa Ester Makassy ALIYEPATA kura 2 .

Kwa nafasi ya Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mhandisi Fatma Ally Rembo ameshinda Kwa kupata kura 178 akifuatiwa na Cartheline Charwe aliyepata kura 79 huku Lilian Mbedule akipata kura 22.

Nafasi ya mkutano mkuu wa CCM Mkoa aliyeshinda Tumain Msowoya Kwa kura 157 akifuatiwa na Diana Kikungwe Kwa kura 77 na Flora Kahangwa kura 31 .

Nafasi ya Baraza la UWT  Mkoa nafasi mbili kila wilaya Kwa  wilaya ya Kilolo   aliyeshinda Leah Mwamoto kura 192 na Monica Mbasha 183 huku  Anna Mlambia akipata  kura 66 Joseph's Kikoti akiambulia kura 26 na Rahabu Mgute aliyepata kura 14 na Rahabu Kuruthum Mbinu kura 14 .

Wilaya ya Iringa Mjini waliochaguliwa ni Lightines Chengula mama Mzungu  Kura 160 na  Shoti kipangula kura 146  huku  Winnie Mtaki akishindwa Kwa kupata kura 75,Elizabeth Mpogole kura 41, Ester Makassy kura 30,  Helmina Mengele Kura 27, Frolah Parangyo kura 12 ,Jesca Nyahoro alipata kura 9 japo alikuwa amejihudhuru.

Wilaya ya Mfindi     waliochaguliwa ni Ester Sanga kura 153,Zeida Sombe Kura 99 huku walioshindwa ni Lyidia Mzema Kura 90,Mara Nguro kura 48,Anna Matemu Kura 31,Getruda Msamba kura 23, Mwanaisha kihombo alijiondoa lakini kapata kura 4 na  Maine's Kiwelu alijiondoa japo alipigiwa kura 2, 


Wilaya ya Iringa Vijijini washindi ni  Halima Mpinge Kura135 na Agape Mahengo kura 92,  huku walioshindwa ni Francisca Sekalinga kura 58,Lilian Mkemwa kura 42,Maulisia Mvila Kura 20 ,Halima Kalenga kura 49,Neema Kibasa kura 11, Delfina Mtavilalo 7. 

Nafasi ya Mjumbe mwakilishi toka UWT  Kwenda UVCCM     aliyechagiliwa ni Lilian Mbedule aliyepata kura 185 huku Maria Sunsu akipata kura 21 ,Diana Kikungwe kura kura 14 na Seki Kasuga na Zena Chatanda waliojitoa kabla ya uchaguzi huo Bado Wajumbe waliwapa kura 3 .

Nafasi ya mwakilishi toka UWT  Kwenda Wazazi mtu mmoja aliyeshinda ni mwanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia kutoka asasi ya Sauti ya Jamii anayefanya vipindi vyake Matukio Daima Tv Jane Mwalembe kura 92 akiwashinda wenzake Hawa Mbegu Kura 73,Diana Kikungwe kura 41 na Joyce Jumbe aliyepata  kura 6
















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS