Header Ads Widget

WAZIRI DKT MABULA AKUTANA NA MEYA WA JIJI LA BUSAN KOREA KUSINI


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (kushoto) akimkabidhi zawadi Meya wa Jiji la Busan Korea Kusini Mhe. Park Heong-Joon Novemba 3, 2022 wakati wa ziara yake nchini humo.

 


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Meya wa Jiji la Busan Korea Kusini Mhe. Park Heong-Joon Novemba 3, 2022 wakati wa ziara yake nchini humo.

                                    XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mhe. Dkt Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jiji la  Busan Metropolitan nchini Korea Kusini Mhe. Park Heong-Joon.

 

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Novema 3, 2022 , Meya wa jiji hilo ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini Korea Kusini baada ya Seoul alionesha nia ya kuendeleza mahusiano baina ya nchi hizo mbili yaliyodumu kwa takriban miaka 30 sasa.

 

Aidha, Mhe. Park Heong- Joon alionesha nia ya jiji lake kuwa na program za kubadilishana uzoefu kwenye nyanja za elimu sambamba na kuwa tayari kusaidia masuala ya miundombinu. Pia Meya huyo wa Jiji la Busan Korea Kusini alionesha nia ya kuja Tanzania kutembelea mbuga za wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara mapema mwakani.

 

Waziri wa Ardhi Dkt Mabula yuko katika ziara nchini Korea Kusini ambapo mbali na mambo mengine  anashiriki  mijadala kwenye maonesho ya maendeleo ya teknolojia ya taarifa za kijiografia - Smart Geospatial Expo 2022.

 

Mwanzoni mwa ziara yake nchini Korea Kusini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na yule wa Ardhi  Miundombinu na Usafirishaji wa Korea Kusini Bw. Won Hee-ryong walisaini makubaliano ya ushirikiano wa  kuimarisha sekta ya ardhi kupitia hati ya makubaliano (MOU) ya ushirikiano kwenye sekta ya ardhi na menejimenti ya taarifa za kijiografia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS