Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Mohamed Bashe amekutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa kilimo Jijini Dodoma.
Mkutano huo uliowakutanisha wadau kutoka AGRA, FEED THE FUTURE, SERA BORA PROJECT, BBT na ASPIRES Umejadili kuhusu ukuzwaji wa sekta ya kilimo kutoka 4% ya hivi sasa hadi kufika 10% ifikapo 2030
Aidha Waziri Bashe amewataka wadau hao kushirikiana kwa pamoja katika maeneo muhimu ili kufikia adhima zaidi katika umwagiliaji, uzalishaji wa mbegu, utafiti, Huduma za ugani na ujenzi wa maghala ili kuzuia upotevu wa mazao baada ya kuvuna
Mbali na hayo waziri Bashe amewashukuru wadau hao kwa Umoja wao mkubwa katika kuonyesha mchango wao mkubwa kwenye suala la kuwakuza vijana kujiajiri kwenye kilimo kupitia mradi wa Building a Better Tommorow (BBT) unaosimamiwa na wizara ya Kilimo.
0 Comments