Header Ads Widget

WAVUVI WAPEWA MAFUNZO MAALUMU YA UOKOAJI KAGERA

 


NA TITUS MWOMBEKI, MATUKIO DAIMA APP KAGERA.


OFISI ya Waziri  Mkuu kitengo Cha maafa imeanza kutoa Mafunzo ya  siku 7 kwa ajili ya kuimarisha ujuzi wa uokoaji kwa vikundi vya maokozi  vya  wavuvi  mkoani Kagera ikiwa Ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya waziri mkuu aliyoitoa  Novemba 7 katika uwanja wa Kaitaba wakati wa kuaga miili ya marehemu 19 waliokufa katika ajali ya ndege.


Hayo yamesemwa na mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya waziri mkuu, Luten Kanali Selestine Masalamado wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa kagera ambapo amesema kuwa  wavuvi 60 kutoka mkoani Kagera  walioshiriki kufanya uokoaji watashiriki mafunzo hayo maalumu kwa kipindi cha  siku 7 ili waweze kuwapa mafunzo na uzoefu kutoka kwa wataalam ili kujua namna nzuri ya kuweza kumuokoa mtu anayepata ajali kwenye maji pamoja na utayari wa kukabiliana na majanga katika ziwa yanapotokea.


Ameongeza kuwa, lengo la mafunzo hayo Ni kupunguza athari zinazojitokeza ziwani, ikiwa ni pamoja na kuokoa maisha ya watu na kupunguza upotevu wa mali wakati wa ajali, huku akisisitiza kuwa mafunzo hayo yatawajengea ujasili wa kukabiliana na majanga yanapotokea katika ziwa Victoria na kuondokana na kasumba ya kusuburi mtu mwingine aje kuokoa wakati janga lishatokea  linapotokea.




Aidha katika siku 7 za Mafunzo wavuvi wametapata vifaa vya uokoaji vitakavyowasaidia kufanya kazi ya uokoaji kwa urahisi pamoja na kujifunza namna ya kuvitumia kuokoa watu ajali inapotokea.


"Nyote mtamkumbuka ajali ilipotokea kila mmoja katika kichwa chake aliwaza afanye Nini ili kuokoa watu ,lazima tujue kwamba katika maswala ya kuokoa unaweza ukapoteza maisha vilevile mfano swala la Maji halina uzoefu mkubwa hivyo Mafunzo ya siku 7 yatawaondole Ile dhana ya kuokoa Kienyeji na kuanza kutumia uzoefu wa Mafunzo katika kufanya uokoaji  wa  watu katika ajali mbalimbali "alisema Masalamando.




Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa shukurani zake kwa ofisi ya waziri mkuu juu ya utekelezaji wa ahadi ya kutoa Mafunzo kwa wavuvi huku akitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuacha tabia ya kubeza juu ya juhudi zilizofanyika katika kipindi Cha ajali hiyo.


"Tuache kubeza kila jambo ,kila kitu ni kujifunza tayari yaliyotokea yametokea na tujifunze zaidi ,wengine mitandaoni wanatumia ajali ya ndege iliyotokea kama sehemu ya siasa ,lakini pia kwa sababu mafunzo yametufikia wanakagera tuyatumie mafunzo haya vizuri na tujikite katika kupunguza ajali zinazotokea majini kila siku kwa kutumia vifaa vyetu vya kusafiria na kusafirishwa mizigo yetu "alisema Chalamila.



Ikumbukwe kuwa ajali ya ndege  iliyotokea Novemba 6 ndani ya ziwa Victoria na kusababisha vifo vya 19  na watu 24 kunusurika.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI