Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa shukurani zake kwa ofisi ya waziri mkuu juu ya utekelezaji wa ahadi ya kutoa Mafunzo kwa wavuvi huku akitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuacha tabia ya kubeza juu ya juhudi zilizofanyika katika kipindi Cha ajali hiyo.
Chalamila amesema "Tuache kubeza kila jambo ,kila kitu ni kujifunza tayari yaliyotokea yametokea na tujifunze zaidi ,wengine mitandaoni wanatumia ajali ya ndege iliyotokea kama sehemu ya siasa ,lakini pia kwa sababu mafunzo yametufikia wanakagera tuyatumie mafunzo haya vizuri na tujikite katika kupunguza ajali zinazotokea majini kila siku kwa kutumia vifaa vyetu vya kusafiria na kusafirishwa mizigo yetu"
TAZAMA FULL VIDEO KUPITIA CHANEL YA MATUKIO DAIMA TV
0 Comments