Header Ads Widget

WATANZANIA WAMETAKIWA KUWA NA TABIA YA KUPIMA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA.

 


NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.

Watanzania wametakiwa kuwa na tabia ya kupima Mara kwa mara magonjwa yasiyoambukiza na kubadili mtindo wa maisha wanaoishi ili kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa Hayo.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kaspar Mmuya wakati akifungua siku ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza Mkoani Mwanza na kueleza kuwa magonjwa hayo yanaweza kuepukika Kwa kubadilisha mtindo wa maisha.


Mmuya Ameeleza kuwa magonjwa Hayo yamekuwa yakisababisha zaidi ya vifo Mil 41 Duniani kote ambapo ni sawa na asilimia 74 ya watu wote wanaofariki duniani kati ya vifo 100 vinavyotokea.


"Sasa hili Jambo ni dogo Kwa kuliangalia na kusikia tu lakini ni Jambo kubwa tunapoteza nguvu kazi ya Tanzania na ukiangalia miaka kuanzia 15-60 wengi wao ndio nguvu kazi wanapata magonjwa hayo na kufariki" Alisema Mmuya.


Amefafanua kuwa katika wagonjwa 100  wanaoumwa hapa Nchini Tanzania vifo 33 husababishwa na magonjwa yasiyoambukiza huku miaka ya 90  waliokuwa wanafariki ni asilimia 20 pekee.


Mmuya Ameeleza kuwa Kila mmoja anapaswa kujikinga na Magonjwa yasiyoambukiza Kwa kufuata njia zitakazosaidia kuishi maisha Bora Kwa kuzingatia ulaji unaofaa, kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, vyakula vyenye chumvi nyingi, vinywaji vyenye sukari nyingi na unywaji wa pombe kupitiliza.


"Mara nyingi mtu anapoenda sehemu kula anakuta chakula kina chumvi lakini bado atahitaji kuongeza sukari ama chumvi hiyo uliyoikuta inatosha na hakuna haja ya kuongeza nyingine"Alisema Mmuya.


Katibu Tawala Msaidizi uchumi na uzalishaji Emily Kasagara ambaye amemwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Elikana Balandya amesema kuwa  Ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza hususani saratani, shinikizo la juu la damu, kisukari na majeraha yatokanayo na ajali yanachochewa na viatarishi vinavyoweza kurekebishika. 


Kasagara amefafanua mtindo wa maisha, matumizi ya tumbaku, unjwaji wa pombe kupita kiasi, lishe duni pamoja na kitojishulisha Kwa kufanya mazoezi Mara kwa mara ndio viashiria vinavyoweza kusababisha magonjwa hayo.


Ameeleza kuwa Utafiti wa mwaka 2018 ulifanyika hapa Nchini ulionesha watu asilimia 8.7 wanatumia tumbaku na mwaka 2012 ulionesha matumizi ya pombe kupitiliza ni asilimia 23.3 na asilimia 34.7 wana unene uliokithiri.


" Hatuna budi kuchukua hatua ili kuepuka madhara makubwa yatokanayo na magonjwa yasiyoambukiza" Alisema kasagara.


Dr, James Charles ni Mwakilishi kutoka wizara ya afya ameeleza kuwa takwimu zinaonesha zaidi ya robo tatu ya watu wenye magonjwa yasiyoambukiza hawajitambui Kama wana magonjwa hayo.


" Ndio maana tunasisitiza utoaji wa huduma ufikie mahali walipo ili waweze kupima na kujitambua wana magonjwa yasiyoambukiza" Alisema James.


James ameeleza kuwa elimu kuendelea kutolewa ili watu waelewe namna ya kujiepusha na magonjwa Hayo yasiyoambukiza na jinsi ya kuweza kuepuka kupata magonjwa hayo.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI