NA HADIJA OMARY, LINDI
KATIKA kuendeleza mapambano dhidi ya Virusi vya ukimwi na UKIMWI na kufikia malengo ya Dunia ya SIFULI TATU ifikapo 2030 bila maambukizi mapya ya VVU na vifo vinavyotokana na UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto Wanasayansi, watoa huduma za afua za VVU na UKIMWI, wametakiwa kuongeza jitihada katika mapambano hayo.
Hayo yamebainishwa na Naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Vijana ,Ajira na watu wenye Ulemavu MHE. PATROBAS KATAMBI katika kongamano la kisayansi lililowakutanisha wataalamu mbalimbali wakiwemo wanasayansi, watoa huduma za VVU na UKIMWI, Wawakilishi ngazi ya jamii zinazotumia huduma hizo pamoja na wadau wa maendeleo lililofanyika jana mjini Lindi.
Kongamano hilo la siku mbili linafanyika chini ya kauli mbiu ya Equalize (Imarisha Usawa), ambalo litatoa fursa ya wadau kujadili mbinu mpya na namna bora ya kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI katika huu muktadha mpya.
Katambi alisema pamoja na kwamba idadi ya maambukizi mapya ya vvu pamoja na vifo vinavyotokana na UKIMWI kupungua sana na Idadi ya Watu wanaoishi na VVU kupata tiba, bado yapo maeneo ambayo juhudi zaidi zinahitajika kuchukuliwa.
Alisema moja ya maeneo yanayohitajika kuongeza jitihada ni pamoja na Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa Mtoto pamoja na Tiba kwa Watoto chini ya Miaka 5.
“Pia kuna baadhi ya makundi yako nyuma katika kufikiwa na Huduma za VVU na UKIMWI kama wanaume, Vijana na Makundi maalumu yalio katika hatari kubwa ya maambukizi ya VVU.”
Kwa upande wake mama kijana kutoka mtandao wa vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi Gea Ramadan alisema ili kumkinga mtoto alie tumboni moja ya mambo ambayo yanatakiwa kufanyiwa maboresho na wizara ya ni swala la Mama kuangaliwa afya yake anapokuwa mjamzito akitolea mfano kwa utaratibu uliopo hivi sasa kuwa mjamzito anapimwa mara moja kwa vipimo vya mwanzoni lakini bila kumbua kwamba mama yule anaendelea kufanya mapenzi ambayo sio salama wa kupi.
“Kwa kuwa mama mjamzito anapimwa mara moja kwa vipimo vya mwanzoni lakini tukumbuke kwamba mama yule anaendelea kufanya mapenzi ambayo sio salama na uwenda anafanya na watu tofauti kwa sababu ya kujipatia kipato na kumuandalia mtoto wake Maisha mazuri hivyo tunapompima mara moja uwenda yule mama hapa katikati akapata maambukizi mapya bila yeye kujua na matokeo yake anamuambukiza mtoto wake” alisema Gea
alisema pamoja na kwamba wanaambiwa wazuie maambukizi mapya lakini wao kama mama vijana ambao wanaishi na maambukizi ndio watu wa kwanza kuleta Watoto wenye maambukizi kunakosababishwa na uwoga wa baadhi yao wa kuweka wazi hali za afya zao kwa ndugu zao wa karibu ama wenza wao
“ sisi tukiendeleza kuzaa Watoto wenye maambukizi tunaona ni kitu ambacho hakitaisha tunaweza tukafika 2030 lakini tusifikie malengo ambayo tunayatamani kuyafikia” alisisitiza Mama huyo kijana.
Naye Meneja jinsia na vijana kutoka USAID Afya yangu kanda ya kusini Abubakari Rahani alisema miongoni mwa shughuli zinazofanywa na USAID katika kushughulika na Waviu ni kuhakikisha wateja wao wote wakiwemo akina Mama wajawazito wanapata huduma zote muhimu anazotakiwa kuzipata .
"Kwanza kama Mama ni Mviu tunahakikisha Mama huyo anapata Elimu ya uzazi pamoja na Afya ya uzazi lakini pia wanapata huduma kulingana na chaguo lake" alisema Rahani.
Akizungumza kwa niaba ya akinamama wanaoishi na virusi vya ukimwi Mwenyekiti wa jukwaa la Wanawake wamaoishi na Virusi vya Ukimwi Jocelyn Mtono alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais samia kwa kuboresha upatikanaji wa huduma kwa akinamama wanaoishi na maambukizi ya VVU hasa katika tiba za uzazi kwani kwa sasa idadi ya Watoto wanaozaliwa na maambukizi imepungua.
0 Comments