Header Ads Widget

SERIKALI KWENDA KUMALIZA UJENZI WA VITUO VYA POLISI MBOKOMU NA URU SHIMBWE VILIVYOANZA KUJENGWA NA WANANCHI.

 



Na WILLIUM PAUL, MOSHI.

VITUO vya polisi vilivyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi katika kata za Mbokomu na Uru shimbwe katika Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani inaenda kuvifanyia tathimini ili kuvikamilisha ujenzi wake.


Akihoji swali la nyongeza Bungeni jana, Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof Patrick Ndakidemi alisema kuwa, wananchi wa kata za Mbokomu na Uru shimbwe wamejenga vituo vya polisi na bado havijakamilika.



Mbunge huyo alihoji Serikali inampango gani kuwasaidia wananchi hao ambao wametumia nguvu zao kujenga vituo na kuwajengea nyumba za mapolisi wa kata.


Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Naibu Waziri Jumanne Sagini alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wananchi na Mbunge huyo kwa ajili ya kuanza jitihada za kujenga vituo vya polisi kwa nguvu zao wenyewe.


Naibu Waziri Sagini alisema kuwa, watawatuma Askari kwa upande wa Kilimanjaro ili kufanya tathimini ya kiwango cha fedha kinachohitajika ili kukamilisha vituo hivyo ambapo wataiingiza kwenye mpango wa ujenzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI