NA AMINA SAID,MATUKIO DAIMAAPP
TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Tanga kuwakamata huku wakisimamishwa kazi ,watuhumiwa wapatao 24 waliojihusisha na kuungua kwa ghala la kuhifadhia mizigo ya TRA katika bandari ya Tanga,ili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.
Mkuu wa mkoa wa Tanga alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya kamati maalumu ya kuchunguza kutokea kwa Moto katika ghala hilo kuanzia tarehe 29 November mwaka huu.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Tanga aliunda kamati hiyo ya uchunguzi mara baada ya kutokea kwa tukio la kuungua moto ghala lenye vitu mbalimbali ambavyo bado havijalipiwa ushuru liliotokea majira ya saa nane na nusu usiku mnamo tarehe 23 October mwaka huu.
Mgumba liwataja badhi ya watuhumiwa ambao wanatakiwa kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ambao ni watumisha sita wa mamalaka ya bandari Tanga ambao ni Bw.Fortunas Sandaria mlinzi wa mwandamizi,Bwa.Aliko Mwakipangala, Bwa.PeterMwankana ,Issa Haruna Abdalah ,James Kyaomoka ,Susan Kanyika mlinzi mwandamizi .
Aidha alisema watumishi wengine ni watumishi saba wa SUMA JKT, Watumishi wa saba wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ,mtumishi wa moja wa TBS ambaye ni mkaguzi wa TBS Tanga wengine ni raia kwaida 3 ambao ni wamehusika kula njama na kuisababishia serikali hasara.
Sambamba na hayo aliwataka mameneja wa Bandari mkoa Wa Tanga na TRA mkoa wa Tanga kutokana na uzembe huo wa taarifa kutofautiana walinzi kupangwa wale wale wajitathimini na kuwajibika.
Aidha aliwaomba Kamishna wa TRA na Mkurugenzi mtendaji wa Bandari Tanzania kuwachukulia hatua watumishi ambao wamegundulika na makosa ya kiutendaji waweze kuwajibishwa.
Awali akisoma taarifa ya uchunguzi wa tukioa la kuungua kwa ghala ya bidhaa na mizigo mbalimbali ya TRA katika Bandari ya Tanga Mwenyekiti wa kamati maalumu Sebastian Masanja alisema kamati iligindua kulikuwa na uwepo wa mkaa nyuma ya ghala ambayo sio kawaida kuwepo kwani hakuna shughuli zygote za mama ntilie iliyowahi kufanyika hapo.
Samabamba na hayo alisema kuwa taarifa ya zilitofautia na kati ya meneja wa TRA na Bandari kwani wanatoa mizigo kwa gets namba moja badala ya geti namba mbili ambapo geti hilo ni la Abiria.
Aidha kamati hiyo ilishauri kwamba Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU jeshi la Polisi waendelee na uchunguzi ili wahusika kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
0 Comments