Header Ads Widget

UVCCM MOSHI VIJIJINI WAMPONGEZA DKT SAMIA...

Na Gift Mongi,Matukio DaimaAPP Moshi 

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima amesema heshima aliyopewa rais Dkt Samia Suluhu Hassan udaktari wa heshima ya juu umekuja muda muafaka kutokana na kazi nzuri alizozifanya kwa muda mfupi.


Akizungumza mjini hapa mwenyekiti huyo amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa alichokaa madarakani na ndio maana wataalam wa elimu na chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)wakaona anastahili kupewa shahada ya juu ya heshima.


Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ni kuwa sio kila mtu anaweza kupata shahada hiyo ya juu ya heshima na kuwa amestahili na kuwa sio kapewa kama rais kwani wapo marais ambao hawajawahi kupewa heshima hiyo.


Shirima amesema kupata heshima hiyo ni matokeo ya kazi ambazo amekuwa akizifanya zenye maslahi mapana ya taifa na ndio maana wataalam katika sekta ya elimu wakaona anastahili na kuwa hiyo ni heshima kwa taifa lakini pia kwa chama cha mapinduzi ambacho pia yeye ni mwenyekiti wake taifa.


Amesema anaungana na vijana wenzake katika wilaya ya Moshi Vijijini katika kumpongeza rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuheshimisha taifa kutokana na utendaji wake ambao umekubalika na unaonekana kwa vitendo kwa kipindi kifupi.


Kwa upande wake wakili Emanuel Mlaki ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi(CCM)amesema kitendo cha rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutunukiwa shahada ya juu ya heshima ni matokeo ya kazi zake zinavyokubalika kwa taifa.


Amesema hadi kufikia hatua ya kupewa shahada hiyo ni ukweli usiopingika kuwa wapo wataalam waliokaa chini na kufanya utafiti na uchambuzi juu ya utendaji wake na hatimaye kujiridhisha kuwa anastahili na kuwa sio kila mtu anaweza kupewa.

Mkuu huyo wa nchi ametunukiwa udaktari huo leo Jumatano Novemba 30, 2022 na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Jakaya Kikwete katika mahafali ya 52 ya chuo hicho yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI