NA AMINA SAID,TANGA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kukamata gari aina ya Toyota Ractis yenye Namba T 515 DXR iliyokuwa ikitumika Kuwaibia watu mbalimbali ,huku likikamata pikipiki 18 zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali ya Jinai.
Akitoa taarifa ya kipindi cha ndani ya wiki mbili juu ya ya misako ya Operesheni iliyofanyika ya mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu mkoani Tanga,Kamishna msaidizi mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe alisema jeshi hilo linaendelea kupambana na uhalifu na wahalifu wanaojihusisha na makosa mbalimbali uliofanyika kwa nyakati tofauti tofauti.
Aidha ailisema kuwa mnamo tarehe 13 Oktoba mwaka huu majira ya saa 11:30 huko maeneo ya Benki ya CRDB iliyopo kata ya central Tarafa ya Ngamiani Kaskazini jijini Tanga ,ilikamatwa gari Namba T 515 DXR aina ya Toyata Ractis na mtuhumiwa alikimbia ambapo mtuhumiwa huwaibia watu mbalimbali kwa utapeli.
Kamanda Mwaibambe alisema kuwa wakati mwingine mtuhumiwa huyo huiba kutoka ndani ya Magari ya wananchi wanaofuata huduma katika benki hiyo,hivyo jeshi la polisi linaendelea kumtafuta ili afikishwe kwenye mikono ya sheria.
Katika hatua nyingine kamanda Mwaibambe alisema kuwa wamefanikiwa kukamata pikipiki 18 katika misako hiyo ya operesheni ya ndani ya mwezi moja ambapo zimekamatwa kwa makosa mbalimbali ya jinai.
Aidha Mwaibambe alitaja idadi ya pikipiki hizo katika misako inayoendelea kuwa ni 18 ambapo kati ya hizo pikipiki 3 zimekamatwa kuhusiana na wizi wa mifugo pamoja na watuhumiwa watatu wilayani Muheza mkoani Tanga.
Sambamba na hayo alisema pikipiki 12 zimekamatwa kwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia nguvu na uporaji wa simu haswa mikoba ya kinamama ambapo watuhumiwa saba wamekatwa watafikishwa mahakamani kuhusiana na tukio hilo.
Hata alisema pikipiki 3 zilmekamatwa kuhusiana na makosa ya usafirishaji wa Dawa za kulevya pamoja na usafirishwaji wahamiaji haramu ambao wameingia nchini bila Kibali.
Katika tukio nyingine alisema jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha bandia katika mkoa wa Tanga ambapo mnamo tarehe 3 Oktoba mwaka huu majira ya saa saba mchana huko katika maeneo ya kisosora kata ya Nguvumali tarafa ya Chumbageni katika jiji la Tanga alikamatwa Huruma John akiwa na silaha(Pistol)bandia iliyokuwa kwenye bagi lake la mgongoni ambapo mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.
Hata hivyo alisema kupitia operesheni hiyo walikamata makosa mengine ikiwa ni pamoja na jumla ya simu 11 smartphone ya aina mbalimbali ,simu ndogo 5 aina mbalimbali ,Laptop 1 aina ya HP, simu 13 aina mbalimbali mifuko 5 ya cement aina ya Huawin, viti 25 Mali ya kiwanda cha cement Rhino watuhumiwa watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.
Aidha Kuhusiana matukio hayo jeshi la polisi mkoa wa Tanga limetoa wito kwa wananchi wote wanaozungukwa na miundombinu mbalimbali pamoja na Hifadhi za wanyama pori kushirikiana kulinda rasilimali hizo ili zilete manufaa kwa Taifa kwa ujumla.
.










0 Comments