Header Ads Widget

NJOMBE DC YAMIMINIWA SIFA NA KIKAO CHA USHAURI CHA MKOA RCC KWA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA KITAIFA KATIKA MASHINDANO YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Kikao Cha ushauri mkoa wa Njombe RCC kimeimwagia sifa Halmashauri ya wilaya ya Njombe chini ya mkurugenzi wake Sharifa  Nabalang'anya na mwenyekiti  Valentino Hongoli kwa kushika nafasi ya kwanza  kitaifa na vijiji vyake viwili vya Image na Ibiki katika mashindano ya afya na usafi wa mazingira.


Akitoa taarifa hiyo mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Zabron Masatu amesema halmashauri ya wilaya ya Njombe imekuwa ikishika nafasi ya kwanza kitaifa kwa miaka kadhaa mfululizo katika mashindano hayo ikifuatiwa na halmashauri ya wilaya ya Makete.


Dkt.Masatu amesema wamepanga kuwafanyia hafla ya kuwapongeza katika siku za usoni kwa kufanya vyema kwa mwaka uliopita huku ushindi wa mwaka huu nao utafanyiwa sherehe zake.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI